salamu kwenu wanabodi.
Viongoz na wanao ongozwa wote tatizo lao ni moja! wanawaza na kutenda kijamaa wakati tupo kwenye mfumo wa kibepari. Na hili limejidhihirisha dhahiri katika awamu hii ya tano kuliko wakati mwingine wowote.Tukijitahidi kutoka katika tope hili tunaweza kupiga hatua kubwa kiuchumi.Nitajitahidi kufafanua kila jambo ili wanajamvi waweze kunielewa.
Tatizo la kuadimika na kupanda bei kwa sukari kwa kiasi kikibwa limesababishwa na serikali. kwanini? serikali inasema inataka kulinda viwanda vya ndani kwahiyo wafanyabiashara wakazuiwa kuleta sukari kutoka nje ya Nchi!Wewe jiulize wale wenye viwanda siyo wafanyabiashara? ni wafanyabiashara.Tena kwakuwa hawako wengi wanaweza kuamua kutengeneza mazingira ya sukari kuadimika ili wapandishe bei kwa visingizi mbalimbali kama kupanda kwa gharama za uendeshaji.Dawa ya kuzuia bei ya bidhaa isipande kiholela ni kuifanya bidhaa hiyo ipatikane kwa wingi kuliko mahitaji ili wauzaji washindane kuuza kwa be inayo vutia wateja na siyo vinginevyo.
Hebu fikiria hivi, kama muagizaji wa madela yale mavazi ya akina mama angekuwa mmoja tu Nchi nzima unajua bei yake ingekuwaje? pengine dela moja lingeuzwa kwa shs 200,000/!! bei ya madela haipandi ovyo kwasababu waagizaji wako chungu nzima kwahiyo bei sokoni imejirekebisha yenyewe wala hatuhitaji EWRA wa mavazi
Kuna jambo baya lina anza kujitokeza sasa mingoni mwetu, nayo ni chuki ya wasio nacho dhidi ya walio nacho.Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa mtazamo wa wasio nacho ni kama wanaona kila mwenye nafuu fulani ya maisha ni fisadi! kulipwa mshahara mkubwa sasa hivi ni dhambi! na ndio maana utawasikia baadhi ya watu wakisema , afadhali sasa tutafanana na heshima itapatikana! wanataka tajiri afanane na masikini badala ya kutamani masikini afanane na tajiri! ndio kuwaza kijamaa.tunawaza juu ya jamii isiyo na matabaka yaani jamii ya watu wasio na uchu wa mafanikio. bila ushindani hakuna mafanikio.Unatamani mtu mwenye Phd alipwe sawa na darasa la saba!