Emmanuel Ndegeya
Member
- Jun 19, 2015
- 46
- 7
Shida ya maji Kata ya Pangani, Halmashauri ya Kibaha Mji Mkoa wa Pwani.
Ndugu Admin/moderator naomba kutoa malalamiko yangu juu ya wizara ya Maji, kwani pamekua na shida ya maji miaka nenda rudi sasa kwa wakazi wa Kata ya Pangani mitaa ya Mtakuja, Kidimu, Pangani yenyewe na mitaa mingine..
Maji mwanzo yalikuwepo na yalikuwa yanatoka angalau mara mbili kwa wiki ila sasa wenye viwanda walifanya lobbying maji yanaishia kwenye viwanda inawalazimu wakazi wakanunue maji kwa magari na wengine inabidi wachote matope waweke cement kuchuja maji.
Wizara ya maji na DAWASA Kibaha waliweka jiwe la msingi kujenga tank upya maeneno ya Pangani ili ujenzi uanze mwezi wa saba ila mpaka sasa hakuna dalili yoyote ile.
Wakazi wanataabika na kero ya maji. Tulikuwa tunaomba angalau wayafungulie yaanze kuwa yanafika kwa wakazi hata mara mbili au tatu kwa wiki ili kunusuru kero ya maji.
Pia soma KERO - Kukosekana kwa huduma ya maji Kibaha - Pangani - Mtakuja kwa miaka minne sasa