Tatizo la taa ya 'oil' kuwaka na kuzima

Oil huwa inapoteza nguvu(viscosity) haipungui.. Ikipungua basi kuna leakage au engine inapata moto mpaka inakausha oil
Hivi kaka mbona kwenye pikipiki zetu huwa tunaweka oil ila mradi iwe ni oil bila ya kuangalia pikipiki inahitaji oil yenye viscosity gani?Ni sahihi kwenye pikipiki kuweka oil yenye viscosity yoyote ile?
 
Pole ndg, nami nina tatizo hilo kwa mda sasa. Juzi nilifanya yafuatayo
1. Service kwa kumwaga oil; tatizo likaendelea kuwepo
2. Kubadirisha switch ya oil; tatizo likaendelea kuwepo
Fundi alikuwa na mpango wa kufungua sample ya oil ili akasafisha chujio; hakufanya hivyo baada ya kugundua/kumwambia sample ilishafunguliwa miaka 5 nyuma baada ya kugonga jiwe na kupata leakage.
Option ya mwisho ni kununua pump; anadai kuwa mzunguko wa oil ni mdogo na hii imejidhiririsha baada ya kukuta oil kidogo sana kwenye oil filter niliyobadirisha.
HITIMISHO; BAADA YA KUPITIA UZI HUU, SITANUNUA PUMP; NITAMSISITIZA TUSAFISHE STRAINER/CHUJIO KWANZA. TAA YA OIL INAWAKA NA KUZIMA
 
Hili tatizo hata mimi ninalo. Nikiendesha umbali fulani , nikikanyaga break taa ya oil inawaka lakini nikikanyaga moto,hiyo taa inaondoka.
 
Mwaka jana nilipata changamoto kama hiyo. Taa ilipowaka, nilisimama nikazima gari. Nilipowasha na kutembea umbali mdogo, taa ikawaka tena, nikaenda kwa fundi. Fundi akasema tutaanza na kusafisha chujio kwenye oil sump, taa isipozimika, tutaangalia zaidi. Oil sump ilifunguliwa na chujio lilikuwa chafu sana, kama tope fulani limejaa. Baada ya kusafishwa, hilo tatizo halikuonekana tena.
 
Pole ndg, nami nina tatizo hilo kwa mda sasa. Juzi nilifanya yafuatayo
1. Service kwa kumwaga oil; tatizo likaendelea kuwepo
2. Kubadirisha switch ya oil; tatizo likaendelea kuwepo....
Kama taa ya oil inawaka na kuzima kwa muda sasa na wewe unaendelea kuendesha gari kwa muda mrefu na taa hiyo kama ulivyojinadi hapa nakuhakikishia kuwa mpaka sasa hivi huna engine!
 
Ushafu kupelekea uchafu kuziba.
Hili nalo linasumbua sana magari ya mjapan
 
Kama taa ya oil inawaka na kuzima kwa muda sasa na wewe unaendelea kuendesha gari kwa muda mrefu na taa hiyo kama ulivyojinadi hapa nakuhakikishia kuwa mpaka sasa hivi huna engine!
Muongo wewe.
Kama engine ingekuwa imekufa gari isingekubali kuwaka na kuingia road.
 
Muongo wewe.
Kama engine ingekuwa imekufa gari isingekubali kuwaka na kuingia road.
Kwani kujua kuwa huna engine ni mpaka upaki gari?Hiyo mbona itakuwa ni late sana!Kuna ubaya wa kujua mapema kuwa huna engine?
 
Hivi kaka mbona kwenye pikipiki zetu huwa tunaweka oil ila mradi iwe ni oil bila ya kuangalia pikipiki inahitaji oil yenye viscosity gani?Ni sahihi kwenye pikipiki kuweka oil yenye viscosity yoyote ile?
Hapana tunafoji tu na kuua engine taratibu bila kujua
 
Mi huwa ina blink hata kama nimetoka kui service sasa hivi.Yaani nimezurura weeh nikajikatia tamaa tu nikasema kama linakufa acha life mradi uhai ninao
 
Naomba kuleta mrejesho kulingana maada tajwa hapo ambayo niliileta kwenu majuzi. Kwanza niwashukuru kwa ushauri wenu hakika umekuwa msaada sana kiasi cha kuniokolea zaidi ya 400,000 maana nilikuwa nimeambiwa na fundi kufungua engine na kununua shaft.

Nilifanyia kazi ushauri wa kusafisha straner na kweli ilikuwa chafu sana tena sana baada ya kusafishwa taa haiwaki tena. Ahsante sana ndugu zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…