Mshasha wane
JF-Expert Member
- Oct 16, 2014
- 231
- 631
Wakuu habari mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa hii forum ya magari japo siyo mchangiaji. Nna gari yangu Toyota Allex jana kuanzia juzi taa ya oil nyekundu kwenye dashboard imekuwa inawaka na kuzima.
Kuna muda nikiwasha gari taa zote za dashboard zinawaka ila yenyewe haiwaki inakuja kuwaka baadae nikiwa naendesha na inaweza kuwaka kwa kucheza cheza (ina blink).
Nimeenda kwa fundi wa kwanza akaniambia issue za shaft na akasema engine lazima ifumuliwe ninunue shaft nyingine. Wa pili akaniambia issue itakuwa oil pump. Naombeni msaada kwa wataalamu wa hivi vyombo maana mimi hii ndo gari yangu ya kwanza kutumia.
MREJESHO:

Naomba kuleta mrejesho kulingana maada tajwa hapo ambayo niliileta kwenu majuzi. Kwanza niwashukuru kwa ushauri wenu hakika umekuwa msaada sana kiasi cha kuniokolea zaidi ya 400,000 maana nilikuwa nimeambiwa na fundi kufungua engine na kununua shaft.
Nilifanyia kazi ushauri wa kusafisha straner na kweli ilikuwa chafu sana tena sana baada ya kusafishwa taa haiwaki tena. Ahsante sana ndugu zangu