Tatizo la miundombinu ya vyoo katika kituo cha mabasi Magufuli laisha. Hatua zachukuliwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,709
13,461
Manispaa ya Ubungo imeona taarifa kuhusu kuvuja maji kwenye mabomba katika kituo cha Mabasi cha Magufuli

Ni kweli changamoto hiyo ipo lakini tumeanza kuchukua hatua.

"Tatizo la miundombinu ya vyoo katika kituo cha mabasi Magufuli limeshaanza kutatuliwa kuanzia leo septemba 30, 2024 mafundi wameanza kufanya marekebisho tangu asubuhi na mpaka sasa hakuna upotevu wa maji kama ilivyokua awali.

Pia, Uongozi wa Kituo unaendelea na zoezi la kubaini maeneo mengine yenye ubovu ili kuthibiti upotevu wa maji lakini pia kuhakikisha miundombinu inakuwa salama

Aidha, uongozi wa kituo unatoa wito kwa wateja wote wa kituo wakiwemo abiria na wafanyabiashara kutumia vizuri miundombinu ya kitu.o hicho kwa ajili ya kutunza hadhi ya kituo hicho kikubwa Tanzania na Afrika Mashariki."

Taarifa hii imetolewa na Joina Nzali Mkuu wa kitengo cha mawasiliano selikalini, Manispaa ya Ubungo.
IMG-20240930-WA0007.jpg
IMG-20240930-WA0008.jpg
IMG-20240930-WA0010.jpg
IMG-20240930-WA0009.jpg
 
Kujisaidia iwe bure.
Ukipanda ngazi kwenda kwenye ofisi za mawakala wa mabasi ghorofani utakutana na harufu ya mikojo kwenye njia za kupita. Wanalipisha vyoo na wakati huo huo wanaacha watu wajisaidie popote na hakuna usafi unaofanywa.
 
Back
Top Bottom