Tatizo la kujikosoa: Vyanzo, Madhara na ufumbuzi wake

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
16,464
35,689
VYANZO VYA TATIZO LA KUJIKOSOA SANA

Mtu ambaye anasumbuliwa na tatizo la kujikosoa sana huwa amepitia historia ifuatayo
Vyanzo vya tatizo la kujikosoa sana ni 3 kama ifuatavyo

1.KUJICHUKIA KWA MUONEKANO
Unaweza kujikuta upo na tatizo la kujikosoa sana, kujilaumu, kujichukia kwa sababu za muonekano wako.
Muonekano wako unaweza kukufanya ujione tofauti na wengine kama upo na mambo yafuatayo
#WANAUME

Kujiona mfupi sana au mrefu sana, kujiona upo na mpangilio usiovutia wa macho,pua, mdomo,meno,kucha,kujiona haupendezi ukivaa nguo yoyote kulinganisha na watu wengine

kuwa na ulemavu wa kudumu, kigugumizi,kujiona mwembamba sana au mnene kupita kiasi,kuwa na maziwa,kuwa na sauti ya kike,kujiona mzee sana kabla ya umri, kujichukia kwa maumbile ya uzazi (kibamia)

Kwa mwanamke

Inaweza kujiona hauna "Shape" kwa maana ukivaa nguo yoyote kulinganisha na watu wengine unajiona haupendezi, kujichukia kwa rangi ya ngozi,kuchukia mpangilio wa viungo mwilini kama pua, mdomo, meno, kucha,nywele n.k

2.KUISHI NA WATU WENYE KUJISIFIA KUPITA KIASI
Unaweza kujikuta upo na tatizo la kujikosoa, kujilaumu, kujichukia, kujiona mkosaji muda wote kwa sababu ya kuzungukwa na mwenza, rafiki, ndugu, mfanyakazi, mwajiri, mwalimu,jirani, mzazi ambaye mara kwa mara anajisifia kupita kiasi kuhusu afya yake, muonekano wake, mafanikio yake, elimu yake,fedha zake,kazi yake , kabila lake, kusafiri sana,kujuana na watu mashuhuri n.k na kukufanya ujione hauwezi kufikia mafanikio yake hata ufanye nini maishani mwako.

Mara kwa mara anadai hauna hadhi ya kuzungumza nae,anadai upo na bahati kuzungumza na yeye,anatishia kukuacha mpweke.

3.KUISHI NA WATU WENYE TABIA YA UKOSOAJI KUPITA KIASI

Vilevile unaweza kusumbuliwa na tatizo la kujikosoa sana, kujilaumu, kujichukia kwa sababu ya kuzungukwa na watu ambao ni wakosoaji kupita kiasi

Anaweza kuwa mzazi,ndugu, rafiki, mwalimu wako, kiongozi wako wa kidini,mwenza wako,jirani yako, mfanyakazi, mwajiri wako n.k ambaye mara kwa mara anadai upo na sura mbaya na hauna "Shape" wala hauna hadhi ya kuzungumza nae,mara kwa mara anakufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina ya udhalilishaji,kukujibu vibaya, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano wako, kukejeli mawazo yako,kudai hauna uwezo wa kiakili wa kujiongoza bila yeye hauwezi kufanikiwa popote.
Hali hiyo husababisha tatizo la kujikosoa, kujilaumu, kujichukia, kujiona mkosaji muda wote.

III.MADHARA YA TATIZO LA KUJIKOSOA SANA

Kwanza kabisa utaishi katika mahusiano yenye manyanyaso miaka yote kwa sababu ukimpata mtu yeyote ambaye anakupenda sana utaibua ugomvi ghafla kwa sababu ya wivu wa mapenzi, vilevile utaogopa kuachwa mpweke hivyo utakuwa king'ang'anizi sana wa mapenzi sehemu ambayo unapigwa vita

Vilevile kazini utafanyiwa vitendo vya udhalilishaji mara kwa mara na utakuwa na hasira kupita kiasi,chuki, kinyongo, wivu na hisia za kisasi.

Unaweza kusumbuliwa na msongo wa mawazo,woga, kutetemeka sana, kuchanganyikiwa kwa vitu vidogo vidogo,kuugua muda mrefu sana bila kupata nafuu, kuugua mara kwa mara,kuumwa kichwa na mgongo na kwa wanawake inaweza kusababisha hedhi kuvurugika au ujauzito kuharibika mara kwa mara kwa sababu ya Stress za mara kwa mara.

IV.UFUMBUZI WAKE
Njia 4 za kukabiliana na tatizo la kujikosoa sana

1.KUPATA UTULIVU WA AKILI

Akili ikiwa na utulivu haijalishi utakosolewa na bingwa wa taaluma gani bado utakuwa na utulivu.Fanya mazoezi ya kupumua (Deep breathing exercises)fanya meditation, vilevile kuna zoezi kama kupiga miayo (Yawning),kupumua haraka haraka kutoa hewa tumboni kuja nje (belly breathing) husaidia kuondoa sauti ya kujikosoa.

Mazoezi hayo hubadilisha sauti inakuwa nzito sana (Deep voice)kwa wanaume na ukiongea unakuwa na mvuto kwa msikilizaji

2.BORESHA NAMNA UNAVYOZUNGUMZA
Simama imara,ukiwa kwenye kiti kaa jaa kwenye kiti tanua miguu sio kukusanya miguu,inua shingo juu sio kuangalia chini kama bibi harusi,tazama usoni mwa mtu yeyote ambaye yupo mbele yako,tanua kifua ,ukianza kuzungumza tumia mikono kueleza tukio ,ongea kwa sauti kubwa sana,epuka kunyenyekea utaonekana DHAIFU SANA mbele ya jamii kisha watakupanda kichwani hata kama hawana faida yoyote kwako

3.WEKA MIPAKA.

Kemea tabia ya watu wengine kukufokea, kukutukana, kukudhalilisha,kukujibu vibaya,piga marufuku mazoea yasiyokuwa na mipaka,sisitiza kuheshimiana na Mwenza wako pamoja na watu wengine.

Epuka tabia ya upole kupita kiasi,epuka uvumilivu kupita kiasi,epuka kusamehe makosa mara kwa mara,epuka kukwepa migogoro,epuka kukaa na kitu rohoni,mtu yeyote akifanya makosa sema moja kwa moja sio kuficha .
Anza kujiona ni kiongozi mkubwa sana popote uendapo watu wataanza kuhisi tofauti wakiwa karibu yako.

4.EPUKA KUJIPENDEKEZA KWA WAKOSOAJI WAKO
Hakikisha mkosoaji wako anakuwa na nia njema kwako kama si mteja wako lakini anakosoa bidhaa zako puuza maneno yake,hata kama ni mtaalamu wa kitu chochote epuka kumnyenyekea kama anatumia lugha ya udhalilishaji kutaja makosa yako au mapungufu yako badala yake mpige marufuku kama hawezi kujiheshimu akae na utaalamu wake.

Boresha mapungufu yako lakini siyo kuwa mtumwa kwa wakosoaji wako kwa sababu ya makosa yako au mapungufu yako.
 
Back
Top Bottom