Tatizo la kuharisha kwa mtoto mdogo

Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,435
1,024
Nina mtoto mdogo Mwenye umri wa miezi mitatu.
Tatizo la huyu mtoto ni kujisaidia kinyesi ambacho kama ameharisha. Wakati mwingine kina kuwa Kama kina majimaji tu au Kama vikambakamba.
Nimeshamtafutia dawa kadhaa ikiwa ni pamoja na kufatilia unyonyshaji wa maziwa ya mama.
Uzito wake umeanza kuwa stagnat kwani alilozaliwa alikuwa na 3.1kg baada ya mwezi na wiki mbili akawa na 5.3kg na mwezi wa pili na wiki mbili akafikisha 6.1kg ila mwezi wa tatu ambao tatizo kulikuwa limesha Anza amefikisha 6.4kg.
kwa sababu tatizo hili limedumu kwa muda Sasa huku tukiendelea kujaribu njia mbalimbali bila mafanikio naomba nililete kwenu ili kwa Mwenye kujua suluhisho au ushauri wa wapi pa kupata msaada anielekeze.
Samahani kwa usumbufu na natanguliza shukrani kwa wewe utakayeguswa.
 
Huyo ni mtoto wa ngapi kulea mkuu, tuanzie hapo kwanza.
Kwa umri huo wa mtoto anaruhusiwa kula maziwa ya mama yake tu, asipewe chochote hata maji ya kunywa, maziwa tu anyonye mara kwa mara.
Kama una mlisha chakula kingine basi achana nacho, tumbo lake halina uwezo wa ku digest hadi afikishe above 6 months
 
Zaidi ya maziwa ya mama yake amekuwa akipewa Lactogen no 1 ila pale tu inapoonekana maziwa ya mama yake hayajamtosha
Huyo ni mtoto wa ngapi kulea mkuu, tuanzie hapo kwanza.
Kwa umri huo wa mtoto anaruhusiwa kula maziwa ya mama yake tu, asipewe chochote hata maji ya kunywa, maziwa tu anyonye mara kwa mara.
Kama una mlisha chakula kingine basi achana nacho, tumbo lake halina uwezo wa ku digest hadi afikishe above 6 months
 
Nina mtoto mdogo Mwenye umri wa miezi mitatu.
Tatizo la huyu mtoto ni kujisaidia kinyesi ambacho kama ameharisha. Wakati mwingine kina kuwa Kama kina majimaji tu au Kama vikambakamba.
Nimeshamtafutia dawa kadhaa ikiwa ni pamoja na kufatilia unyonyshaji wa maziwa ya mama.
Uzito wake umeanza kuwa stagnat kwani alilozaliwa alikuwa na 3.1kg baada ya mwezi na wiki mbili akawa na 5.3kg na mwezi wa pili na wiki mbili akafikisha 6.1kg ila mwezi wa tatu ambao tatizo kulikuwa limesha Anza amefikisha 6.4kg.
kwa sababu tatizo hili limedumu kwa muda Sasa huku tukiendelea kujaribu njia mbalimbali bila mafanikio naomba nililete kwenu ili kwa Mwenye kujua suluhisho au ushauri wa wapi pa kupata msaada anielekeze.
Samahani kwa usumbufu na natanguliza shukrani kwa wewe utakayeguswa.

Pia wakwangu anashida hiyo naomba kuju wako ulifanyaje
 
Mara nyingi, choo Cha watoto huwa chepesi hasa hao wadogo.... Kwahiyo unapaswa kujua tofauti iliyopo kati ya mtoto kuharisha na kuwa na choo chepesi....

Cha kusisitiza...
1. Kunyonyesha au unyonyeshaji wa maziwa ya mama mara kwa mara, yanasaidia katika kuongea kinga na kupunguza baadhi ya changamoto hasa kwa watoto...
Na ndio maana tunasisitiza unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa muda usiopungua miezi 6

2. Mazingira na usafi...
Hapa wengi wanashindwa kutekeleza hili, unakuta mama katoka kufanya shughuli zake anafikia kumnyonyesha mtoto maziwa angali chuchu hajazisafisha

Lingine ni kuhakikisha tuna nawa mikono Kila wakati na kuhakikisha tunaosha vyombo ambavyo vinatumiwa na watoto wachanga ili kupunguza baadhi ya changamoto...

TUJITAHIDI KUPUNGUZA MATUMIZI YA DAWA KWA WATOTO WACHANGA (MATUMIZI YA DAWA HASA KWA MAGONJWA AMBAYO YANAWEZA KUZILIKA HASA MAGONJWA YA KUHARA)

NASISITIZA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA KWA KIPINDI CHA MIEZI 6 MFULULIZO

asante
 
Back
Top Bottom