Tatizo la gari kuchanganya oil na maji

wa ukwee

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
260
73
Habari wana jamvi,

Naomba kwa wenye ujuzi na uzoefu wa magari tusaidiane mawazo. Toyota vanguard inachanganya maji na oil. Kabla ya kufikia hatua hii ilikua inakula oil sana, kabla ya kilomita 3000 nusu ya oil imepotea.

Juzi imeanza kuwa na miss sana ikitembea kama 5km inazima. Leo nimecheck oil nakuta imepanda sana, ndio nikagundua inachanganya na maji.

Nimemcheck fundi anasema hapo ni kununua engine nyingine. Naomba wenye uzoefu tusaidiane mawazo, nikifanya overhaul gari haiwezi kukaa sawa?

Hakuna option zaidi ya kununua engine nyingine.

Nawasilisha kwa ushauri wenu wadau
 
Habari wana jamvi
Naomba kwa wenye ujuzi na uzoefu wa magari tusaidiane mawazo. Toyota vanguard inachanganya maji na oil. Kabla ya kufikia hatua hii ilikua inakula oil sana, kabla ya kilomita 3000 nusu ya oil imepotea.
Juzi imeanza kuwa na miss sana ikitembea kama 5km inazima. Leo nimecheck oil nakuta imepanda sana, ndio nikagundua inachanganya na maji.
Nimemcheck fundi anasema hapo ni kununua engine nyingine. Naomba wenye uzoefu tusaidiane mawazo, nikifanya overhaul gari haiwezi kukaa sawa? Hakuna option zaidi ya kununua engine nyingine.
Nawasilisha kwa ushauri wenu wadau

Kusema moja kwa moja shida nini si rahisi.

Inawezekana kuwa issue ya head gasket, seals za oil cooler, turbo charger (kama ipo) au hata cylinder head.

Ni aina gani ya gari?

Vipi ina chemsha?

Hata hivyo ufumbuzi kamili, fika kwa mafundi magari wa maana, tu.

Hilo ni known problem, halina ugeni.
 
imeunguza silinder head gasket.

mwambie fundi afungue akapime silinder head kama haijaumia sana ipigwe kisu kidogo ununue gasket mpya ufunge

pia kwakua inakula oil utabadilisha block slive silinder, piston ring na valvu sil

pia ucheki radiator Yako eiza inavuja au nichafu ndio inaweza kua imesababisha gari kuchemsha

asante
 
Kusema moja kwa moja shida nini si rahisi.

Inawezekana kuwa issue ya head gasket, seals za oil cooler, turbo charger (kama ipo) au hata cylinder head.

Ni aina gani ya gari?

Vipi ina chemsha?

Hata hivyo ufumbuzi kamili, fika kwa mafundi magari wa maana, tu.

Hilo ni known problem, halina ugeni.
Jibu zuri hata mimi akili yangu ya haraka iliwaza kwenye Head gaskets na Gaskets za oil cooler...
 
Kusema moja kwa moja shida nini si rahisi.

Inawezekana kuwa issue ya head gasket, seals za oil cooler, turbo charger (kama ipo) au hata cylinder head.

Ni aina gani ya gari?

Vipi ina chemsha?

Hata hivyo ufumbuzi kamili, fika kwa mafundi magari wa maana, tu.

Hilo ni known problem, halina ugeni.
Gari ni toyota vanguard ya 2009. Inachemsha mkuu, na ukiongeza maji hayavuji mahali lakin huyaoni pia kujaa
 
Gari ni toyota vanguard ya 2009. Inachemsha mkuu, na ukiongeza maji hayavuji mahali lakin huyaoni pia kujaa

Kwa vyovyote inabidi uende garage. Haitakuwa rahisi kwako kurekebisha hili mwenyewe.

Kuna sehemu 2 za kuangalia kwenye oil cooler (rahisi) na kwenye cylinder head (costly).

Kutegemeana na historia ya tatizo na tahadhali zozote zilizochukuliwa wakati wa tatizo kutaamua mwelekeo.

Kama gari imeachwa ku overheat tegemea habari mbaya, levels tofauti za uharibifu, na hata matengenezo na gharama zaidi.

Matatizo kama yako huanza kidogo kidogo kwa kuchemsha ikisababishwa na very minor failures.

Tofautisha kuchemsha na ku overheat.

Tayari uko na idea, nenda garage ukaanze hata kwa kuwasikiliza kikomavu ukaleta mrejesho, ushauri wa bure mbona tutakupa tu mkuu?
 
Back
Top Bottom