Quartz360
Senior Member
- Mar 27, 2023
- 133
- 315
Tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa ni kilio kwa vijana walio wengi, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia kumi 10% tu ya wahitimu huweza kupata ajira rasmi kila mwaka. Huku asilimia 90% wakibaki bila ajira rasmi.
Tatizo hilo limeibua fursa kwa upande wa makampuni, Biashara binafsi, NGOs na mashirika. Ambapo kwa kiasi kikubwa wamekuwa hawatoi ajira tena badala yake wanatembea na kile wanachokiita VOLUNTEERING na INTERNSHIPS. Kwa malipo kiduchu ama hakuna kabisa ukilinganisha na kazi wanazofanya vijana hao. Na hilo limefanya vijana wengi wasiwe na chaguo, badala yake wanaona ni bora wakafanye hizo Internships ama kujitolea ili tu siku ziende kwa kuwa ajira imekuwa ni kilio cha taifa.
Mbaya zaidi waajiri wao pia wamekuwa na kiburi kwa sababu vijana wako wengi mtaani, anaweza kukufukuza leo, kesho akapata mwingine.
Very Sad.