Tatizo kubwa la usafiri Dar inawezekana ni idadi kubwa ya watu na jiografia ya mji ilivyokaa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
46,838
67,234
Dar es Salaam, asubuhi karibia theluthi mbili ya wakazi wote wa mji wanaofanya kazi wanaenda Kariakoo, Posta na Ubongo katika maofisi, kwenye biashara na pia kufuata huduma mbalimbali za kiofisi, halafu jioni tena karibia watu wote hao wanageuza kurudi makwao kwa pamoja kama kumbi kumbi.

Kwa jinsi hii ukichanganya na matatizo mengine ya kukosa ufanisi katika miondombinu ya barabara za kawaida na mwendokasi jiji lazima likabiliwe na matatizo makubwa ya usafiri.
 
Maendeleo ya jiji yakiwq na kitovu ndo inavyokuwaga. Majiji yote yenye kitovu yanahangaika na shida ya usafiri. Asubuhi kuwapeleka watu mjini na jioni kuwarudisha. Kesi ya usafiri dar ni kesi ya Center basing development. Na majiji yote yenye maendeleo ya hivyo ndo shida hiyo ipo
 
Sio too late, bali itahitajija gharama kubwa sana na akili kubwa mno kurekebisha.
Kwa population ngumu sana. Eneo dogo la square km 1,600 na population ya Mil 8? Unategemea muujiza gani hapa mkuu. Yaani pop density ya 3,100 people per km sqr.
 
Mimi huu ni mwaka wa nne sasa kwenda kkoo labda iwe bidhaa ambayo mahali pengine sitapata, naweza kaa hata miezi 6 sijakanyaga.
 
Sio too late, bali itahitajija gharama kubwa sana na akili kubwa mno kurekebisha.
Mkuu waka sio Gharama!
Nakupa hii!
1.Ingefanyika Soko ka Kariakoo Haswa Maduka ya Bidhaa kujengwa kati ya Mlandizi na Ruvu/Chalinze,Mbona Bandari Kavu inawekwa Sijui Soga Vipi itashindikana hili?
Unakuwa Umefanya Equally distribution of assets and resources. Sababu Ingekuwa Rahisi Kuweka Miundombinu kuelekea huko, Tayari kuna Mwendokasi hadi chalinze,Barabara za Kuingia na Kutoka zingekuwa nyingi tuu sababu Nafasi ipo.Kariakoo imeshakuwa Exhausted na Miundombinu!

2.Soko la Vyakula tuu ndio Libaki Kariakoo
Hii Ingepunguza sanaa Msongamano wa Watu na magari kaka!
 
Dar es Salaam, asubuhi karibia theluthi mbili ya wakazi wote wa mji wanaofanya kazi wanaenda Kariakoo, Posta na Ubongo katika maofisi, kwenye biashara na pia kufuata huduma mbalimbali za kiofisi, halafu jioni tena karibia watu wote hao wanageuza kurudi makwao kwa pamoja kama kumbi kumbi.

Kwa jinsi hii ukichanganya na matatizo mengine ya kukosa ufanisi katika miondombinu ya barabara za kawaida na mwendokasi jiji lazima likabiliwe na matatizo makubwa ya usafiri.

Tatizo la kuwepo kwa janga la Usafiri na Usafirishaji katika Mji wa Dar es Salaam ni kutokana na KUKOSEKANA KWA MIPANGO-MIJI katika Mji huo, na hata katika Miji mingine yote iliyopo Tanzania na nchi yote kabisa kwa ujumla.

Kumbuka: Msingi Mkuu kabisa wa Ujenzi wa nchi yoyote ile hapa duniani huanzia na suala zima la kuanzisha na kutekeleza Miradi ya Mipango-Miji pamoja na Upimaji Ardhi katika nchi husika. Utawala wa nchi ukishindwa kuanza kujenga nchi kwa kuanzia na hatua hizi za Mipango-miji na Upimaji Ardhi, basi automatically kwenye nchi hiyo upo uwezekano mkubwa sana kwamba watashindwa kupanga vizuri mipango mingine yote kwenye nchi hiyo.

Maendeleo katika nchi yoyote ile hapa duniani huanzia na hatua hizi za Mipango-miji na Upimaji wa Ardhi.
 
Sio too late, bali itahitajija gharama kubwa sana na akili kubwa mno kurekebisha.
Sasa ninyi wa Daslam mjengewa flyover, barabara njia nne, mwenda Kasi, mabasi ya kila Aina, n.k, n.k lakini bado mnaa shida ya usafiri.
Sisi wa Kazuramimba-Kigoma tuna basi moja Tu la kutupeleka mjini. Ukichelewa Hilo inabidi usubiri ili usafiri kesho yake. Barabara yetu ni ya vumbi.
 
Back
Top Bottom