Bando la wiki
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 835
- 2,809
Mwisho wa mwaka huo unaelekea ukingoni. Leo tutaangalia baadhi ya wanasiasa waliojitahidi kuzingatia miiko ya siasa kwa kutanguliza maslahi ya raia (wananchi) mbele bila kuzingatia maslahi yao binafsi kwanza.
Nchi ya Tanzania ina viongozi wengi wa siasa ila ni maskitiko makubwa kwamba wengi wao wanawaza utajiri wao binafsi kuliko wananchi waliowapa dhamana ya kuwa hapo walipo kwenye viti vya enzi.
Bila kuzingatia vyama vya siasa hawa ni viongozi bora wa siasa ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya watanzania kwa hali za kipekee.
1. TUNDU ANTIPAS LISSU
Huyu mwamba ndie anaeongoza kwenye list hii. Uimara wake kuwapigia wananchi wa Tanzania ni wa miaka na miaka pasipo chembe chembe za rushwa wa kulambishwa asali.
2. JOHN HECHE
Huyu pia yumo kwenye list kutokana na uimara wake na misimamo yake isiyo yumba pale anapopambania wananchi.
3. JAJI JOSEPH WARIOBA
Mzee huyu ni tofauti na wastaafu wengi walioko nchi hii, wastaafu wengi viongozi walioko nchi hii wakisha hakikishiwa ulaji na vipesa na vicheo kwa watoto wao hawana uwezo wa kukemea hata mambo maovu yanayoweza kuondoa misingi ya uhuru na demokrasia katika nchi hii. Kwa Mzee jaji Warioba hilo jambo haliwezekani kuanzia enzi za Kikwete akiwa rais, aliweza kupitisha rasimu bora ya katiba ya nchi yenye mapendekezo muhimu kutoka kwa wananchi kinyume na matakwa ya serikali. Kwenye awamu ya tano na ya sita bado anakemea mambo ambayo yanadidimiza utawala bora nchini.
3. JERRY SLAA
Huyu kijana nae kwenye uongozi wake anatenda kwa hofu ya Mungu na kutanguliza maslahi ya wananchi mbele kabla ya maslahi yake binafsi. Ukitaka kuona hofu yake ya Mungu na wananchi mtazame alipokuwa waziri wa Ardhi alijitahidi sana kupambana na mapapa yaliyokuwa yanahodhi ardhi za maskini nchi hii.
4. DR. EMMANUEL NCHIMBI
Huyu mzee ana hekima sana japo yupo kwenye chama kile kisijojali sana malalamiko ya wananchi ila from bottom of his heart unaona kabisa ana kauli za kuponya maumivu ya watanzania. Check speech zake kwenye kifo cha mzee Ali Kibao unaona kwamba anaguswa na maumivu ya wananchi wanaopitia madhira hao tofauti na kiongozi mmoja mkubwa ambaye yeye alidai kifo ni kifo tu.
5. LUHAGA MPINA
Huyu jitihada zake kuipigania Tanzania mpya ziko wazi kabisa. Kumbuka suala la DP WORLD kupata tenda ya kuendesha bandari ya Dar es salaam pasipo kushindanishwa na makampuni mengine yeye ndie aliyekuwa tofauti na wabunge wote mle bungeni kupinga upatikanaji wa tenda hiyo kwa DP world. Bado sakata la sukari tuliona namna alivyo simama imara sema tu mifumo ya rushwa ndio iliingilia kati kumdhibiti lakini bado dhamiri yake ni pana katika kuleta uwajibikaji serikalini.
6. PAUL CHRISTIAN MAKONDA
Huyu jamaa ni mtu anayejitahidi sana kuwa pamoja na wananchi wake. Unakumbuka aliweza kuwapa platform wadudu na jamii nyingine nyingi zinazodharaulika katika jamii ili na wao wajione ni watu wa muhimu katika jamii. Changamoto yake ni kutaka kujipendekeza kulikopita kiasi kwa kiongozi wake mkuu ili aonekane ndie mchapa kazi kuliko watumishi wake wote hapo ndipo anapokosea kwa sababu ni bora utende kwa busara za kimungu kuliko kujipendekeza kwa mwanadamu mwenzako ili kupata vyeo vya kidunia hii vinavyo baki hapa duniani pindi unapofariki.
7. FREEMAN MBOWE❌❌
Huyu mwanzoni alikuwemo kwenye list ila kitendo cha kuchukua fomu ili kuongoza chama katika cheo alichokaa kwa zaidi ya miaka 20, kunamuondolea heshima ya kuwa mwanasiasa bora 2024.
Taja mwingine aliyesahaulika au ambaye hastahili kuwemo kwenye list