Taswira ya nchi yetu kimataifa imechafuka sana ndani ya kipindi cha miezi miwili iliyopita kuliko wakati mwingine wowote tangu 2021, na tunakoelekea inaonesha hali itakuwa tete zaidi.
Suluhisho sio matumizi ya nguvu za dola, suluhisho ni masikilizano.
Ili maridhiano kati ya chama tawala (CCM) na vyama vya upinzani yaweze kuzaa matunda ni wakati muafaka kwa viongozi wetu kuunda serikali ya mpito kuelekea uchaguzi wa 2025. Serikali hiyo ijumuishe viongozi kutoka upinzani.
Jambo hili litawapa nafasi viongozi wa upinzani kushirikiana na wale wa chama kimoja na kufanya maamuzi ambayo yataunganisha nchi yetu na kuleta uelewano na umoja kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Ni vyema sasa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais ikaundwa na wakapewa wapinzani, pia nafasi ya Naibu Waziri Mkuu ipewe wapinzani. Baadhi ya nafasi za uwaziri zipewe viongozi wa vyama vya upinzani pia. Hayo yamefanyika Zanzibar na hata Kenya pia na yamesaidia kuleta usawa na kuheshimiana zaidi kati ya vyama vyenye itikadi tofauti.
Iundwe tume huru kweli kweli ya uchaguzi la sivyo nchi itachafuka zaidi kabla na baada ya uchaguzi 2025. Nashauri pia rais afanyie kazi malamiko ya wapinzani na watu wa jamii mbalimbali wakiwepo Wamasai kuhusu haki na demokrasia.
Kupuuzwa kwa malalamiko haya kwaweza kuipeleka nchi yetu kwenye machafuko ambayo hakuna kiongozi au mtu yeyete ameweza kufikiri ingewezekana.