Jana tarehe 23/12/2023 siku ya Juma mosi nilitembelea maeneo ya Kiluvya Gogoni kuanzia kituo cha Polisi hadi Shule za kata za Hondogo kwakweli barabara ni mbovu sana!! Je? TARURA Wilaya ya Ubungo huwa mnapita maeneo hayo au mnakaa tu ofisini?.
Eneo hilo ni muhimu sana liwekwe lami kwani wanafunzi wetu maeneo hayo wanapata taabu lakini pia wakazi na shughuli za kiuchumi.
Wananchi wanafahamu kwa Rais Samia kamwaga Mabilioni kwa TARURA ili kujenga barabara muhimu za mitaani, barabara hii ya kiluvya /hondogo kuelekea Shule za Sekondqri Hondogo ni muhimu ijengwe kwa lami.
Tofauti na TARURA za wilaya zingine nadiriki kusema kuwa TARURA Wilaya ya Ubungo Mmelala.
Wilaya ya Ubungo iko nyuma sana katika ujenzi wa Miundombinu ya barabara ukilinganisha na wilaya zingine.
Ukiangalia hata mradi wa DMDP wilaya zingine umefanya kazi kubwa lakini katika wilaya ya Ubungo hamna kitu.
Watendaji jikiteni kutazama maeneo ya pembezoni ili kutatua kero zinazo wakabili wananchi.
Kazi iendelee.......