TARURA: Barabara ya Goba Wakorea hadi Tegeta itakuwa ya lami, njia za watembea kwa miguu na taa za barabarani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kutaka kujua mrejesho kuhusu Jenzi wa baraba ya Tegeta kwenda Goba Wakorea umefikia wapi, TARURA wasema mchakato unaendelea.

TARURA wamesema Barabara hiyo ya Goba Wakorea itakuwa ya kiwango cha lami ambapo ujenzi huo utakuwa na njia za watembea kwa miguu na taa za barabarani.

"Barabara hii ya Goba Wakorea (TegetaA) km 7.8 ipo katika mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami ambapo ujenzi huo utakuwa na njia za watembea kwa miguu na taa za barabarani kupitia mradi wa DMDP II kwa Wilaya ya Ubungo. Wamesema TARURA.

TARURA wameiambia Jamiiforums kwamba, Mradi huu kwa sasa upo katika hatua za mwisho za manunuzi kwa maana ya kufanya tathimini ya kumpata Mkandarasi atakayefanya kazi hii .

"Kazi hii itaanza mara baada ya kukamilisha kwa hatua za manunuzi kwa kusaini mkataba na Mkandarasi," ameongeza TARURA.

Pia, soma:
~
KERO - √ - Barabara Tegete A ni kero, kama wameshindwa kuboresha watuambie Wananchi tujichange
~ Barabara Tegete A ni kero, kama wameshindwa kuboresha watuambie Wananchi tujichange
 

"Barabara hii ya Goba Wakorea (TegetaA) km 7.8 ipo katika mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami ambapo ujenzi huo utakuwa na njia za watembea kwa miguu na taa za barabarani kupitia mradi wa DMDP II kwa Wilaya ya Ubungo." - TARURA

Nimekaa Paleeeee :FeelsKinkyMan:

 
Back
Top Bottom