Tarimo Nemes, anayedaiwa alifariki akiwa vitani Ukraine, aligombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia CHADEMA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580
Taarifa za Mtanzania, Tarimo Nemes Raymond kudaiwa kufariki zimewashtua wengi, hasa baada ya kuanza kusambaa mitandaoni huku kukiwa hakuna taarifa rasmi juu ya tukio hilo.

Tetesi zilizosambaa mitandaoni zinaeleza amefariki kwa kuuawa katika vita nchini Ukraine ambapo Tarimo inaelezwa alikuwa akiisapoti Urusi katika vita hiyo dhidi ya Urusi.

Hadi sasa Januari 20, 2023 hakuna tamko la Serikali wala mamlaka zozote rasmi kuhusu taarifa za msiba huo.

Nyumbani kwao Tarimo wameshaweka msiba maeneo ya Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar es Salaam, wakiwa wanasubiri taratibu nyingine kwa kuwa mwili bado haujaletwa Nchini.


IMG-20230117-WA0028.jpg
WAZEE WALIOMLEA RATIMO NEMES
Wazee hao ambao wamejitambulisha kuwa Nemes alikuwa akiwachukulia kama babu na bibi wanaeleza:

Tumemfahamu Tarimo kuanzia akiwa na umri mdogo, mama yake alikuwa msichana mdogo wakati anampata Tarimo.

KUHUSU MAMA TARIMO
Tulikuwa tunaishi jirani na mama yake, tulizoeana kwa kuwa sisi ndio tulimtafutia kiwanja akajenga nyumba ambayo ndio walikuja kuishi baadaye, hivyo akawa jirani yetu wa karibu.

Mama yake Nemes Tarimo ilitokea akaugua siku moja tu na kufariki siku hiyohiyo, akamuacha Nemes akiwa anaingia kidato cha kwanza.

Bahati mbaya baba mzazi wa Nemes pia alifariki muda mrefu kabla ya mama mzazi wa Nemes kufariki, wawili hao walibahatika kuwa na mtoto mmoja tu ambaye ndiye huyo marehemu.

Mama yake alikuwa mjasirimali, kutokana na kazi zake kuwa nyingi akamuomba mke wangu (hapa anatambulika kama bibi wa marehemu) ili awe anakaa na mtoto na amtafutie shule.

Hilo walilifanikisha na Tarimo akapelekwa shule ya bweni, Tosa Maganga ya Mkoani Iringa, akasoma huko kuanzia darasa la kwanza hadi alipohitimu la saba.

Alipotoka hapo akaenda kusoma Bagamoyo elimu ya Sekondari, ni wakati huo ndipo mama yake alipofariki, ikabidi tuendelee kuwa chini ya uangalizi wetu licha ya kuwa alikuwa akiishi kwenye nyumba ileile ya mama yake.

Alipohitimu elimu ya sekondari akaenda kusoma Chuo cha CBE, alipohitimu akapata kazi, baadaye akaenda Urusi kwa leno la kujiendeleza kimasomo.

Nemes234.jpg

Picha ya mwisho aliyopost Nemes katika ukurasa wake wa Facebook mnamo Januari 8,2021.

UTATA WA KIFO CHA TARIMO
Taarifa za msiba tulianza kuzisikia juujuu baadaye mjomba wake (Andrew) akaja na kutuambia kuwa taarifa hizo ni za ukweli.

Mara ya mwisho tumewasiliana na Nemes ilikuwa Septemba 2022, alipiga simu tukaongea naye na akawa anawapa maelekezo mafundi wa ujenzi kwa kuwa alikuwa anaiboresha nyumba aliyokuwa anaishi (iliyojengwa na mama yake).

NEMES ALIRUDI KUGOMBEA KIBAMBA
Ni kweli alikuwa na mpango huo wa mambo ya siasa na ndicho kitu ambacho kilimrudisha hapo katikati.

Kwani Nakumbuka alitoka Tanzania na kwenda Urusi kwa ajili ya kusoma, akiwa huko akaunganisha kufanya kazi hukohuko.

Wakati wa uchaguzi alirudi kuja kugombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA, baada ya kumalizika kwa uchaguzi akasimama kwa muda kutokana na CORONA kisha baadaye akaondoka tena kurejea Urusi.

Nemess.jpg

Nyumbani kwa Tarimo, Mbezi Kibanda Cha Mkaa, nyumba ambayo alipanga kuifanyia maboresho kabla ya kurejea Nchini.

TAARIFA ZA TARIMO KUSHIRIKI VITA
Tumeshtuka na hatuna uhakika kama kweli alishiriki katika vita, kwa kuwa hata mgambo tu hajapita.

TABIA ZA TARIMO
Alikuwa kijana mpole, hakuwa mtu wa makundi, muda mwingi aliutumia akiwa na laptop yake chumbani. Akiamua kutulia unaweza kuhisi hayupo kumbe yupo ndani katulia tulii.

Hakuwa na kawaida ya kutembelewa na marafiki au wageni, zaidi ni wale ndugu wachache ambao wanajulikana fulani na fulani zaidi ya hapo hakuwa mtu wa kujichanganya.

MJOMBA WA MAREHEMU (Andrew Mwandeluka)
Taarifa za msiba tulianza kuzipata mwanzoni mwa Januari kupitia kwa dada yake ambaye alijulishwa na marafiki wa Tarimo lakini hatukuambiwa kuhusu chanzo cha kifo wala kuelezwa amekufaje.

“Tunasubiri tamko la Serikali, tunawasiliana kupitia ubalozi, wamesema Ijumaa hii (Januari 20, 2023) ndio watatupa taarifa juu ya ujio wa mwili na huyo atakayekuja na mwili ndio atakuwa na ripoti kamili.

“Mara ya mwisho nilizungumza naye Novemba 2022, tulizungumza mambo ya kifamilia tu, akasema anataraja kurejea Nchini Februari 2023.

TAARIFA KUWA ALIKUWA MFUNGWA
Hizo taarifa sina na sijawahi kusikia, ndiyo kwanza nazisikia.

KINACHOFUATA
Tunasubiri mwili wake ufike kisha mambo mengine yataendelea.


KUWASILIANA NA FAMILIA
Mara nyingi alikuwa anapiga simu yeye, ukimpigia hata kama hatapokea au hapatikani anakutafufa yeye baadaye.

DADA YAKE NEMES (SALOME KISALE) ANAJIBU MASWALI

Nemes alikuwa mtu wa aina gani?

Hakuwa mtu wa makundi au starehe, pindi anapokuwa nyumbani alikuwa akipenda kukaa ndani muda mwingi, alikuwa anajisomewa. Alikuwa na marafiki lakini hakuwa siyo kivile.

Tangu aondoke mara nyingi yeye ndiye alikuwa anapiga simu lakini hapo kati hatukuwa na mawasiliano naye.

Nini kimemuua ndugu yako?
Kuhusu ndugu yetu amekufaje tunasubiri tamko la Serikali kupitia Ubalozi wa Urusi wao ndio watatupa taarifa rasmi.

Kwani aliwahi kuwa na matatizo na mtu yeyote Tanzania au Urusi?
Hakuwahi kutuambia kama alikuwa na tatizo lolote na mtu au maisha yake yalikuwaje huko Urusi, hatuwezi kuongea vitu ambavyo hatuvifahamu.

Tunatoa shukrani kwa Rais Samia kuitia wateule wake, tumepata msaada mkubwa kupitia Ubalozi wetu uliipo Urusi, Balozi ametusaidia sana kuhakikisha mwili unarudi Tanzania, ndio maana tunasubiri tamko lao baada ya mwili kuja.

Nani alikuwa wa kwanza kupokea taarifa ya msiba wa Nemes?
Mimi ndio nilianza kupata taarifa kupitia kwa marafiki zake waliopo Urusi. Walisema tunasikia Nemes amekufa na kututaka kufuatilia, ndipo tukaanza kufuatilia ubalozini.

Tulipowasiliana na Ubalozi wakasema wanafuatilia baadaye wakatuambia ni kweli lakini taarifa nyingine zitafuata.

Maziko yatafanyika wapi?
Mwili utakapofika tunatarajia kuusafirisha hadi Mbeya kwenda kumzika alipozikwa mama yake.

Nemes aliwahi kupitia mafunzo yoyote ya kijeshi?
Hapana, hatukuwahi kuona wala kusikia kuhusu hilo. Sisi familia hatujui lolote kuhusu hilo.

Alikuwa na umri gani?
Alizaliwa mwaka 1989.


Pia, soma:
Mtanzania Tarimo Nemes Raymond, afariki akiwapigania Wagner wa Urusi, kule Ukraine
FB_IMG_1674238162553.jpg
FB_IMG_1674238172279.jpg
FB_IMG_1674238165819.jpg
FB_IMG_1674238177141.jpg
FB_IMG_1674238239443.jpg
FB_IMG_1674238285539.jpg
FB_IMG_1674238221606.jpg

Picha za Tarimo enzi za Uhai wake
 
Poleni sana wafiwa.

Nimeumizwa sana na msiba wa Huyu mtanzania Mwenzetu.

Japo Kuna UTATA kwamba Alikwenda Urusi kama Mwanafunzi Alikwenda kimasomo.

Sasa hizi habari za kuwa ni Mwanajeshi, alijiunga na jeshi, Amefika jeshini kwa kweli zinatuogopesha sana.

UKWELI UNAWEKA HURU.
 
Hapo kwenye kujulikana aligombea ubunge kupitia chadema moja kwa moja kunamtoa kuwa raia stahiki anayetakiwa kuzungumzwa/kutolewa taarifa na serikali ya CCM.

Inaenda wiki ya pili sasa tangu taarifa hizi zisambae ni nini kinachofanya isitoke taarifa rasmi kumuhusu?
 
Hapo kwenye kujulikana aligombea ubunge kupitia chadema moja kwa moja kunamtoa kuwa raia stahiki anayetakiwa kuzungumzwa/kutolewa taarifa na serikali ya CCM.

Inaenda wiki ya pili sasa tangu taarifa hizi zisambae ni nini kinachofanya isitoke taarifa rasmi kumuhusu?
Huko Chadema mlimshindanisha na Tumbo Tumbo!
 
PoleniI sana Bavicha

Mgombea ubunge anafariki lakini chama hakina taarifa yoyote?

Halafu wanataka wakabifhiwe nchi nzima

Chadema ni bure kabisa
Kama familia yenyewe haina taarufa kamili unaanzaje kukilaumu chama, hapa wa kulaumu ni serikali siyokua na taarufa za raia wao
 
Hapo kwenye kujulikana aligombea ubunge kupitia chadema moja kwa moja kunamtoa kuwa raia stahiki anayetakiwa kuzungumzwa/kutolewa taarifa na serikali ya ccm.

Inaenda wiki ya pili sasa tangu taarifa hizi zisambae ni nini kinachofanya isitoke taarifa rasmi kumuhusu?
Kwa hiyo hata wale waliopigwa risasi Afrika ya Kusini nao serikali imekaa kimya kwa sababu walikua wanachadema?

Tuache siasa kwenye uhai wa raia wetu
 
Huko Chadema mlimshindanisha na Tumbo Tumbo!
Mimi hayo ya kushindanishana siyajui kinanishangaza mimi kwanini serikali isitoe tamko kuhusu mwananchi wake aliyefariki Russia?

Mbona akifa mtoto wa kiongozi au kiongozi mwenyewe akifia India taarifa hutolewa mapema huyu nini kinazuia?
 
Kwa hiyo hata wale waliopigwa risasi Afrika ya Kusini nao serikali imekaa kimya kwa sababu walikua wanachadema?

Tuache siasa kwenye uhai wa raia wetu
Wao hao serikali ndiyo wanaoleta siasa!

Wakifa wao India au UK hawajaingizwa kwenye jokofu tayari huku breaking news kila mahali shughuli zinasimama ila wakifa wengine kimya kwanini?serikali ina double standard waache otherwise hatuwezi kusema siyo siasa.
 
Back
Top Bottom