Mcheza Viduku
JF-Expert Member
- Jun 24, 2020
- 1,087
- 2,664
Wandugu wapendwa wana Jf happy fulishi dei, Mama anaupiga mwingi.
Tuje kwenye mada sasa maana mi sipendagi mambo ya kusalimiana salimiana huwa inaleta ka unafiki.
Mara ya kwanza; miaka kadhaa iliyopita katika tarehe hii hii inayoitwa siku ya wajinga, nikapigiwa simu na jamaa yangu akanipa taarifa za kwamba wanahitajika mabondia kwa ajili ya kujiunga na jeshi (enzi hizo nilikuwa nafanya mazoezi ya ubondia na timu ya jeshi) natakiwa niwahi kambi ya jeshi pale nyegezi kona Mwanza kabla ya saa 4 asubuhi.
Kufupisha stori, niligandishwa pale hadi saa 6 mchana ndio nikastukia mchezo.
Mara ya pili; nilikuwa kwenye hali ngumu sana kiuchumi, saa 11 alfajiri jamaa yangu askari wa wanyamapori akanipigia simu ananiambia nisubiri hapo barabarani nakupitishia nyama ya porini njoo na mfuko mkubwa, niliganda pale hadi saa 4 asubuhi nilikuja kustuka baada ya kusikia watu wanaongelea siku hii.
Mara ya tatu; ilikuwa mwaka jana tu jamaa yangu aka-edit sms ya M pesa halafu akanitumia akaniambia nikaitoe kabla ya saa 4......unaambiwa hadi nilikorofishana na mawakala zaidi ya watatu.
Vipi kwako mwananzengo mwenzangu tangu huyu mjinga aliyebuni hii siku ushawahi kudanganywa mara ngapi na ulidanganywa kuhusu nini.