Frajoo
Member
- May 28, 2024
- 12
- 3
Salamu;
Moja ya sekta nyeti inayogusa kila mwananchi ni sekta ya Afya, lakini ndio sekta isiyojitosheleza zaidi kwa miaka mingi hususani maeneo ya vijijini.Natambua juhudi za Serikali za awamu zote katika kuongeza idadi ya vituo vya Afya vijijini na mijini pamoja na kujitahidi sana kuingiza nchini vifaa tiba vinavyoendana na wakati.Pia taasisi na asasi zisizo za kiserikali nazo bega kwa bega zimekua chachu ya kuongeza na kuboresha huduma za Afya nchini.
Lakini ni ukweli usiopingika kwamba bado changamoto ni nyingi dhidi ya maongezeko na maboresho hayo, hususani maeneo ya vijijini ambako idadi kubwa ya wananchi ni wa hali za chini kiuchumi wasiomudu swala la usafiri kufuata huduma bora za afya.
Japo Waziri Ummy Mwalimu alinukuliwa akisoma ripoti kwamba zaidi ya asilimia 74 ya watanzania wanapata huduma za afya ngazi ya msingi, kwa mwaka 2023 mahudhurio ya wagonjwa yameongezeka hii ina maana wanapata huduma zinazoridhisha.Lakini ukizuru vijijini kama mimi nilivyopata uzoefu utagundua changamoto ni kubwa kwa maeneo yasio na vituo vya afya.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO ,utafiti wa ripoti inabainisha wazi kwamba “huduma ya msingi ya afya kuelekea huduma ya afya kwa wote unakadiria kwamba takribani maisha ya watu milioni 60 yanaweza kuokolewa kwa kuongeza matumizi ya huduma za msingi za afya katika nchi za kipato cha chini na cha wastani kwa dola bilioni 200 kila mwaka”
Hivyo basi, japo kwa ujumla huduma za afya zimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2000 ,ripoti hiyo ya huduma za afya kwa wote (UHC) inaonesha pengo kubwa la huduma za afya katika nchi masikini.Huku maeneo ya vijijini yakiwa na kawaida ya kuwa na huduma za afya hafifu, kutokana na miundombinu mibovu,upungufu wa wafanyakazi na huduma duni za afya.
Vijiji vya Tanzania vina bahati mbaya hata ya kukosa wakupaza sauti kwa wakati.Ukweli wanao Maafisa afya wanaotembelea kutoa huduma panapotokea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na zaidi, huko ndipo wanakutana na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa maeneo husika.
Sote tunafahamu kwa nchi masikini kama Tanzania sio ndoto ya usiku mmoja kujenga hospitali za rufaa ,za wilaya ,vituo vya afya ,zahanati nchi nzima huku huduma zikitolewa kwa urahisi na gharama nafuu.Ni wazi miundombinu ,vifaa tiba na kuajiri wafanyakazi ni gharama kubwa japo wahisani na taasisi nyingi zinaisaidia Serikali lakini bado tupo nyuma.
MAONI YANGU.
Nadhani jambo la kufanya kwa wakati huu ni kuhakikisha serikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi pamoja na wahisani wanapeleka huduma za msingi za afya vijijini ili kuelekea dhamiri ya huduma ya afya kwa wote.
Kivipi? Natamani kuona Tanzania ina vituo vya afya mzunguko.(Mobile Health Centres.) Ni magari maalumu ambayo yataandaliwa kubeba vifaa tiba ya msingi, watoa huduma wabobezi,huduma ya choo na huduma zingine sanjari.Badala ya kujenga vituo 6 kwenye vijiji 12 ,yapelekwe magari mawili ambayo yataweka kituo kijiji kimoja kwa siku kadhaa kulingana na uhitaji.Serikali za mtaa ndio jukumu lake kuwatangazia wananchi. Wataalamu wanapo g’amua mgonjwa anahitaji matibabu zaidi ataandikiwa aende hospitali ya wilaya au ya rufaa kama ilivyo kawaida kwa vituo vya afya.
Kwa magonjwa baadhi wananchi wasitozwe chochote ili kupata vipimo na matibabu mfano TB HIV/AIDS na mengineyo ,hio itachochea wananchi kujitokeza kupata huduma pasi na shaka yeyote kwasababu ni gari.
Kwa mahudhurio ya wagonjwa ambao wanahitaji mrejesho juu ya maendeleo yao kiafya ,nadhani haitakuwa zoezi gumu kuweka ratiba vizuri ili kuhakikisha kila baada ya kipindi fulani kituo kitawafuata,uzuri watadahamu kituo kinachofuata ni kijiji fulani hivyo ni rahisi kufuata huduma kama kuna uhitaji wa dharula.
Hii haina maana kwamba tuache kujipanga ili kujenga vituo vya afya vya kudumun katika maeneo husika.La hasha hii itapunguza vifo vinavyotokana na kuchelewa kupata huduma za afya vijijini, kama inavyoripotiwa mara kwa mara wajawazito , watoto hata watu wazima huwa katika hatari ya kupoteza maisha au kupata tatizo la kuduma kwasababu ya kuchelewa kupata huduma ya afya kwa wakati.
Magari ya dharula ya wagonjwa (Ambulance) mara nyingi yanahitajika vijijini kwasababu ya kuchelewa kupata huduma ya afya ,kwahiyo Kituo cha afya mzunguko ni mrobaini wa changamoto hii ,pengine tukapunguza kwa asilimia kubwa idadi ya wagonjwa mahututi vijijini.
Pengine gharama za ujenzi wa vituo 6 vya afya kwenye Wilaya moja (jambo ambalo utekelezaji wake utachukua miaka mingi) Serikali inaweza ikapata magari hayo maalumu mawili ambayo kimsingi yanaweza kuzungukia vijiji vyote.
Inawezekana. Wazo hili nililipata baada ya kuona gari kubwa lililokuwa linatoa huduma ya vipimo vya TB mkoani Arusha.Nikawaza kwanini isiwe magonjwa yote ?Kwanini lisiweke kituo eneo moja hata Juma zima? Kwanini wananchi hawajatangaziwa kwa msisitizo jambo hili lijulikane ili watu wajitokeze? Nadhani kwa Serikali itaweza kufanya matangazo vile inafaa ili kila mwananchi afahamu kuna Mobile Health Centre kwenye eneo lake.
Hili ndilo tamanio langu kuona Tanzania mpya inawarahisishia wananchi hasa waishio vijijini wapate huduma ya afya yenye ubora na kwa urahisi na gharama nafuu.
Asanteni sana kwa muda wenu.