JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,775
- 6,592
Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na athari zozote za kimazingira wakati wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga kwani tahadhari zote zilizingatiwa kitalaamu.
Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 16, 2022 ikiwa ni sehemu ya ufafanuzi ya maazimo yaliyotolewa siku tatu na Bunge la Ulaya (EU) kuhusu utekelekezaji wa mradi huo.
Kwa mujibu wa DW, bunge hilo linatoa maazimio ikionyesha athari baada ya kampuni ya bima Allianz Group, benki 15 na kampuni saba za bima (HSBC, BNP Paribas na Swiss Re) kukataa kutoa ufadhili wa kifedha kwa mradi huo kufuatia kampeni inayoendeshwa na kundi la kimataifa la 350.org.
Siku tatu zilizopita Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limetoa maazimio saba ikiwamo madai ya mradi huo kutozingatia viwango vya kimataifa katika kulinda haki za binadamu na mabadiliko ya Tabianchi, kutolipa fidia huku likishinikiza kulinda haki za wanaharakati wa mazingira,
“Wito kwa EU na jumuiya ya kimataifa kutoa shinikizo kubwa kwa mamlaka za Uganda na Tanzania, pamoja na waendelezaji wa mradi na wadau, kulinda mazingira na kukomesha shughuli za uchimbaji katika mazingira yaliyohifadhiwa na nyeti, ikiwa ni pamoja na pwani ya Ziwa Albert,”ilinukuu taarifa.
“Kujitolea kutumia njia bora zaidi kuhifadhi utamaduni, afya, na mustakabali wa jamii zilizoathiriwa na kutafuta njia mbadala kulingana na ahadi za kimataifa za hali ya hewa na bayoanuwai; wito kwa waendelezaji wa mradi kutatua migogoro yote iliyopaswa kutatuliwa kabla ya uzinduzi wa mradi huo.”
Pia Bunge hilo limeagiza kuzingatia hatari zote zinazotishia mradi huo, ikiagiza Total Energies kuchukua mwaka mmoja kabla ya kuzindua mradi wa kusoma uwezekano wa njia mbadala ya kulinda vyema mifumo ikolojia inayolindwa, nyeti na rasilimali za maji za Uganda na Tanzania.
Aidha, pia bunge hilo limeagiza kupunguza hatari ya kuathirika kwa mabonde ya maji katika ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika, ambayo ni rasilimali muhimu kwa kanda, na kuchunguza miradi mbadala kulingana na nishati mbadala kwa maendeleo bora ya kiuchumi.
Msimamo wa Serikali
Hata hivyo akitoa ufafanuzi juu ya wasiwasi huo, Makamba katika taarifa yake ya maandishi alinukuliwa akisema Mfumo wa kisheria na kibiashara wa bomba hili umeanzishwa katika Makubaliano ya mkataba kati ya mwekezaji na Nchi husika (HGA) yaliyotiwa saini Mei 20, 2021 kati ya Serikali na EACOP.
“HGA inaweka wazi uhusiano kati ya EACOP na Serikali ya Tanzania katika masuala kama vile Ardhi, viwango vya HSE (Afya, usalama, ulinzi, mazingira), utawala wa fedha, Uidhinishaji na taratibu za migogoro. Mamlaka ya Serikali ya kufuatilia mradi huu ni Ewura na NEMC,”amesema Makamba.
“Kilomita 1,147 za bomba zitakazojengwa Tanzania pamoja na temino na 4 vituo vya kusukuma maji. Bomba linahitaji upana wa mita 30 wa kulia wa njia, Bomba la kuzuia mivujo na joto la nje litajengwa kina cha mita moja, baada ya ujenzi udongo wa juu na mimea itarejeshwa na ardhi itafikiwa na watu na wanyama.”
Katika ufafanuzi wake, Makamba bomba litafuatiliwa na kebo ya hali ya juu inayoweza kugundua mabadiliko ya halijoto na mitetemo katika urefu wote wa bomba.
Amesema hakuna ardhi itakayochukuliwa na mradi bila kufanyiwa fidia zinazokadiriwa kuwa Sh23bilioni kwa wakazi 9,122.
“Utwaaji ardhi unazingatia Sheria zote mbili za Tanzania na Viwango vya Utendaji vya Shirika la Fedha la Kimataifa. Tanzania wapo Watu 9,513 walioathiriwa na mradi na 331 za kuhamishwa kwa chaguo la makazi au fidia ya pesa taslimu. Takriban asilimia 85 yao wamechagua kwa makazi na ujenzi unaendelea.
Chanzo: Mwananchi