Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,052
- 23,501
Wakuu,
Tanzania imeendelea kung'ara kwenye utalii katika ngazi ya kimataifa na hii ni baada ya kuibuka kidedea kwa mara nyingine tena kwenye tuzo za World’s Leading Safari Destination
=============================================================
Hatimaye baada ya mchuano mkali Tanzania imeibuka kuwa eneo linaloongoza zaidi duniani kwa utalii wa safari (hasa za kuona wanyama wa porini) ikiyashinda mataifa mbalimbali duniani ikiwemo nchi za Afrika, hii ni kwa mujibu wa Tuzo za Utalii Duniani (World Travel Awards) zilizotolewa usiku wa kuamkia leo yaani jana Novemba 24, 2024 kisiwani Madeira, Ureno.
Zikitambulika kuwa sawa na “Tuzo za Oscars” katika tasnia ya utalii, World Travel Awards (WTA), ndio tuzo za juu zaidi duniani na tangu mwaka 1993, zimekuwa zikitambua mafanikio na umahiri katika ngazi ya mabara na kidunia katika kategoria anuai za utalii.
“Tunawashukuru wote waliotupigia kura kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwemo wadau wa utalii na uhifadhi wenye hadhi ya kupiga kura lakini na mtu mmoja mmoja walioichagua Tanzania"
“Tuzo hii ni ushahidi wa matokeo ya uhifadhi wetu mkubwa uliofanywa na viongozi wa awamu zote na unaoendelezwa katika Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia na uwekezaji mkubwa tunaoendelea nao katika kutangaza utalii kwani wengi walioipigia kura Tanzania maana yake ni wazi walitembelea na kuridhika na umaridhawa na uasili wa hifadhi zetu,” alisema Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, aliyeongoza msafara kupokea Tuzo hiyo hapa Madeira.
Kwa mafanikio hayo Rais wa WTA Bw. Graham Cooke pia ameitangaza Tanzania kuwa mwenyeji wa Tuzo za Utalii Duniani Kanda ya Afrika mwaka 2025.