BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,818
Makubaliano hayo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amezipongeza timu za wataalam wa nchi hizo mbili kwa kazi ya kuongoza majadiliano yaliyowezesha kukubaliana na kusainiwa kwa Kumbukumbu za Majadiliano hayo, ambazo zinaelezea ushirikiano wa nchi hizo kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Bw. Mwandumbya, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani kwa ahadi ya msaada huo utakaozinugausha sekta za maendeleo nchini katika eneo la Bioanuwai, ambalo kwa kiasi kikubwa linajumuisha kusaidia Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Wanyamapori ili kuhifadhi mazingira yake tajiri ya asili na kuongeza mapato kupitia utalii endelevu, pia katika Sekta ya Afya ambayo inajumuisha maeneo ya Huduma za Dharura za Watoto Wachanga, Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango kwa vijana, na Bima ya Afya ya Pamoja.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa uju shukrani zangu za dhati kwa msaada huu ninawahakikishia kwamba, Serikali ya Tanzania itafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba fedha zinatumika kama ilivyokusudiwa” alisema Bw. Mwandumbya.
Aliongeza kuwa ahadi zilizotajwa zitasaidia miradi maalum ikiwemo wa Kupunguza Migogoro baina ya Binadamu na Wanyama, kiasi cha Euro milioni tisa (9); Mradi wa Maendeleo Endelevu ya Mifumo ya Hifadhi, kiasi cha euro milioni 15, Mradi wa Kuimarisha Afya ya Uzazi na Kuwawezesha Vijana wa kike, kiasi cha euro milioni tisa na Mradi wa Kuimarisha Mfumo wa Bima ya Afya wa kwa Wote nchini Tanzania, kiasi cha euro milioni tatu (3).