Tanzania Yapiga Kura Kuunga Mkono Azimio la Umoja wa Maifa Kuitaka Israel Ijitoe Haraka Iwezekanavyo Gaza

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
61,743
72,153
My Take
Tanzania imeendelea kutuma ujumbe Kwa Mabeberu hasa USA kwamba hatupangiwi na hatuchaguliwi rafiki.

Tanzania imepiga kura kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa linaloitaka Israel kumaliza uwepo wake "usio halali" katika eneo la Gaza.

Azimio hilo, lililopitishwa siku ya Jumatano, linaitaka Israel kujiondoa kutoka Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki ndani ya mwaka mmoja huku mgogoro na Hamas ukikaribia kutimiza mwaka mmoja mnamo Oktoba 7.

Azimio hilo, ambalo ni la kwanza kuandaliwa na Palestina katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA), lilipitishwa kwa kuungwa mkono na nchi 124.

Hatua hii inafuatia uamuzi wa ushauri wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) uliotolewa mwezi Julai, ambao ulisema uwepo wa Israel katika maeneo ya Palestina ni kinyume cha sheria.

Soma Pia: Tanzania yapiga kura za mkutano mkuu UN Kupinga vita ya Israel-Gaza

Hongera sana Rais #SSH# Kwa msimamo thabiti.
Snapinsta.app_460104457_3006946866128234_4826162071940661343_n_1080.jpg
 
Toka Kwa Mwalimu Nyerere Tanzania iliunga mkono palestina, lakini pia tuliunga mkono Biafra ijitenge kutoka Nigeria, tulivunja mahusiano na morroco, japo wamerudi majuzi tu hapo, Tanzania ni wajamaa ambapo mrengo huo ndio palestina alikua akiufuata
 
Toka Kwa Mwalimu Nyerere Tanzania iliunga mkono palestina, lakini pia tuliunga mkono Biafra ijitenge kutoka Nigeria, tulivunja mahusiano na morroco, japo wamerudi majuzi tu hapo, Tanzania ni wajamaa ambapo mrengo huo ndio palestina alikua akiufuata
Maazimia ya miaka ya karibuni tulikiwa tuna absteen ila Sasa tumeamua kuwa wawazi.

Misaada haiwezi kutuamulia Cha kufanya.
 
Back
Top Bottom