Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,660
World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

20230624_211152.jpg

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
 
That's a good thing.... in so far as Tanzania has to offer not so good when it comes to exposure....

Jiulize nchi kama UK ingekuwa na good weather na mazingira mazuri yenye marashi ya mimea na maliasili unadhani kuna mtu angetoka kwenye kisiwa chao ?

Migration nyingi apart from economical nyingine ni political... niambie hizo nchi zinazoongoza takwambia kwanini ?

Anyway apart from uongozi mbovu Tanzania still has a lot to offer you can squeeze opportunities here and there.... Just turn a blind eye kwa upuuzi wa hapa na pale....
 
Watz wengi kwa akili zetu fupi tunafikiri kuwa na diaspora wengi ndio mafanikio.

Ni kweli kuna changamoto katika taratibu za kutoka nje. Pia kuna shida na tabu nyingi ndani ya nchi hii, zikichangiwa zaidi na mfumo wetu wa kiutawala.

But all in all, we should thank God a thousand times for the way we are. Ukitaka kuelewa kidogo tu Tz tulivyo safi vuka border hapo Sirari uone maisha yalivyo tofauti kule utakakoingia, hata salamu utatamani uinunue.

Kuna watu humu juzikati nimeshangaa kuona wakiwasifia Somalia kwa kuwa na diaspora wengi, huku wakiwish nasi tuwe kama Somalia! Wonderful!
 
World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

View attachment 2667693

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
Inawezekana pia ikawa inaongoza kwa raia wake wengi kutokuwa na passport.
 
Roho mbaya ya utawala ndo kisa.
Passport tu kuipata mpaka uulizwe tupe letter mfano ya chuo unachoenda. Na chuo unachoomba hawakupi letter wanataka uwape passport number ili waandike letter. Sasa wangapi watatoka?

Chuo wanakuomba maombi yako ili wayafikirie wanataka barua ya TCU kwamba una qualify kusoma hicho ulichoomba, unakimbia TCU kuwaomba barua, wao TCU wanakwambia ili wakuandikie wanataka admission letter ya hicho chuo.
Ni kweli kabisa, Passport ni haki ya kila raia ila nchi yetu kuna bureaucracy ya hali ya juu saana kupata hiyo passport
 
I'm proud of my country,japo hatupo exposed na hatuna elimu sana ila hua nakubaliana kua most of the times ignorance is bliss. Ujinga wetu ni faida sana kwetu.

Watanzania ni watu flani hivi maskini jeuri and I proud of that. Japo hatuna pesa ila hatushoboki Kwa watu,pia hatupendi kulia Lia njaa.
 
Back
Top Bottom