Tanzania yahimiza ushirikiano nchi za SADC katika usimamizi wa Misitu ya Miombo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
WhatsApp Image 2024-04-17 at 10.44.53_baaf0dc0.jpg
Serikali ya Tanzania imezihimiza nchi za ukanda wa SADC kushirikiana katika usimamizi wa Misitu ya Miombo kutokana na umuhimu wake kiuchumi, kijamii na katika uhifadhi mazingira.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 17,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu usimamizi endelevu wa misitu ya miombo unaofanyika jijini Washngton DC nchini Marekani.

“Tushirikiane na kupeana uzoefu, mbinu na teknolojia bora za usimamizi na uendelezaji wa misitu ya miombo" Mhe Kairuki alisema.

Aidha, Kairuki amezitaka nchi hizo kushikamana kwa pamoja kukabiliana na kasi kubwa ya uharibifu wa misitu unaotokana na shughuli za kibinadamu kama vile ukataji miti, kilimo, uchomaji moto na utegemezi wa nishati ya kuni ” Waziri Kairuki amesisitiza.
WhatsApp Image 2024-04-17 at 10.44.53_560b9482.jpg

WhatsApp Image 2024-04-17 at 10.44.51_3b1a7bd2.jpg
Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ametaja jitihada mbalimbali za Serikali ya Tanzania katika usimamizi na uendelevu wa misitu ya miombo kama mpango wa kitaifa wa kuhamia kwenye nishati safi kutoka katika matumizi ya kuni na mkaa ambapo kufikia mwaka 2031 Tanzania iwe imeshahamia kwenye matumizi ya nishati safi.

Pia amesema Tanzania inaendelea kuimarisha viwanda vya mazao ya nyuki kwa ajili ya kuwezesha wafugaji wa nyuki kupata fedha na hivyo kupunguza utegemezi kwenye misitu.

Ameomgeza kuwa pia Tanzania inaendelea kuimarisha usimamizi wa sheria katika misitu na kuhimiza ushiriki wa jamii katika uhifadhi wa misitu ikiwa ni utekezaji wa Sera ya Taifa ya Misitu.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri, Wabunge na Maafisa Waandamizi kutoka nchi za Zimbabwe, Zambia, Namibia, Msumbiji, Malawi, Congo, Botswana, Angola na Tanzania, Umoja wa Afrika na wadau mbalimbali wa uhifadhi.
 
Back
Top Bottom