Kila inapofika tarehe 8 mwezi wa 3 duniani kote huazimisha siku ya wanawake, hii ni njia ya kuwatambua na kuwathamini wanawake katika kila hatua ya msaada na mchngo wao kwa jamii na katika nchi ya Tanzania hasa serikali hii ya awamu ya tano yenye dira ya kujaza viwanda Tanzania ili kujenga uchumi wa kati na kuondoa Tatizo kubwa la Ajira nchini Tanzania.
Iili kukidhi kauli mbiu ya hapa kazi tu katika kuazimisha siku hii ya wanawake dunian imekuja na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda, wanawake ni msingi wa mabadiliko lengo kubwa ni kuwawezesha wanawake katika nyanja ya elimu, mitaji, Biashara na mambo mengine mengi ili iwe chachu ya maendeleo ya viwanda.
Nichukue fursa hii kuwapongeza wanawake kwa kazi nzuri wanayofanya katika jamii kwa kututunza kutuvumilia wanaume kwa kila hatua tunayopitia hakika hakuna kama mama pongezi zangu za dhati ziende kwa mabinti zetu, dada zetu, mama zetu kwa ujumla mungu awainue.