Tanzania ya viwanda imegeuka ya matamshi.

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,803
Serikali imepiga marufuku mwanafunzi yeyote kukariri/kurudia darasa kwa kigezo cha kufeli/kukosa wastani. Barua iliyosainiwa na Kaimu Kamishna wa Elimu Ndg.Nicolas Buretta imezipiga marufuku hata shule binafsi kuweka mchujo kwa wanafunzi wao. Kwa barua hii ni kwamba hata mwanafunzi akipata wastani wa 00% aruhusiwe kuendelea na kidato kinachofuata. Katika kusisitiza hilo Burreta amesema shule yoyote itakayobainika kuchuja wanafunzi wake kwa kigezo cha wastani itachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufungiwa.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Baada ya serikali kuharibu kabisa elimu kwenye shule zake, sasa inapanga kuharibu na shule binafsi pia. Serikali ya CCM inafanya juhudi kubwa sana kuua elimu nchini. Baada ya kuzorotesha elimu ktk shule bora za serikali kama Ilboru, Kibaha, Tabora boys &girls, Ruvu, Weruweru etc, sasa wanajipanga kuua bora za shule binafsi kama St.Francis, Mirian, Tusiime, Majengo sec Moshi, Maua Seminary etc kwa kuzilazimisha ziondoe mchujo kwa wanafunzi wao.

Yani mama Ndalichako na watendaji wake wameona njia nzuri ya kuboresha elimu ni kulazimisha shule binafsi kufuta mchujo? What a shame? Hivi shule binafsi zikifuta mchujo itakuaje? Kinachofanya hizi shule binafsi angalau ziendelee kufanya vizuri ni kwa sababu ya mchujo. Na wanafunzi hujitahidi kusoma kwa bidii sababu ya kuogopa mchujo. Sasa serikali inalazimisha mchujo ufutwe. Ili iweje?

Yani logic ya kuondoa mchujo ni nini? Au ni ili watoto wa viongozi ambao ni mambumbumbu waweze kusoma na kumaliza bila bugudha? Huu ni ijinga usiovumilika. Nashauri shule binafsi zisikubali ujinga huu. Kwanza hakuna mzazi anayelazimishwa kumpeleka mwanae shule yenye mchujo. Kama umeona shule ina mchujo mpeleke mwanao shule nyingine isiyo na mchujo.

Napinga kwa nguvu zote huu ujinga wa serikali wa kulazimisha shule binafsi zifute mchujo. Na ninatoa rai kwa wamiliki wa shule hizo kukataa ujinga wa aina hii. Ulimwengu wa leo ni wa ushindani (survival for the fitest), kama huna nguvu huwezi kusurvive. Wakati wenzetu wanashindana kwa nguvu, sisi tunataka kutengeneza mazingira ya hovyo yanayoruhusu usawa kati ya genius na mbumbumbu?

Hivi mwanafunzi anayepata wastani wa 12%, ukimruhusu asichujwe apite hadi form four na amalize, utathubutu kumuita msomi? Ataweza kushindana na wenzie wa level hiyo katika nchi jirani kama Kenya, Uganda etc? Mbona mama Ndalichako alifanya vizuri sana alipokua NECTA sasa hivi kala maharage ya wapi? Mbona watanzania tulimwamini sana alipoteuliwa tukijua ataboresha elimu, sasa anatuprove wrong?

Nashauri Mchujo uendelee. Kama waziri, mbunge, mkurugenzi etc anaumia kuona mwanae amechujwa pale Tusiime, au psle Mirian, itz better amtafutie shule nyingine sio kulazimisha shule kufuta mchujo. Zipo shule nyingi tu ambazo hazina mchujo, ampeleke huko.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…