Gambino X
Member
- Aug 20, 2014
- 75
- 104
TANZANIA TUITAKAYO 💪🏽.
Tanzania ya VIJANA wenye uelewa wa shughuli KUU za kiuchumi zilizo katika maeneo yao wanayoishi au kuzaliwa ambazo zina wawezesha kujiajiri au kuajiriwa katika makampuni au taasisi zilizopo kutokana na mazingira yanayo wazunguka kama bandari, kilimo, uvuvi, madini, utalii, makampuni ya usafirishaji na mawakala wa forodha……
Kupelekea Kuijenga Tanzania yenye MIJI (Cities) endelevu na VIJANA wengi watendaji ambao wana uwezo na Ufahamu wa jinsi ya kusajili vikundi na/au kuanzisha kampeni na kampuni zenye tija na uwezo wa kufanya biashara hadi nje ya mipaka (export).
TATIZO……😡
Vijana wengi wa Tanzania wamekua wakiishia form 4 na kushindwa kuendelea na elimu zaidi kutokana na sababu nyingi zikiwemo za Kiuchumi yani kukosa Ada na pesa ya matumizi kutokana na kupangiwa mbali na mkoa wake / nyumbani…. afya na familia.
Hivyo ndoto nyingi za vijana hawa huishia tu mtaani na kubaki na sintofahamu ya maisha yao… kati ya hawa vijana wengine ni walikua smart sana darasani na hata kufaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo…
KINACHOENDELEA…. kilio😭
Vijana hawa WANAPOTEA sana kwa KUKOSA MAARIFA…..wapo waNAOshawishika na kuanza kufanya shughuli za uovu kama uporaji, ujambazi na hata kujiingiza katika makundi ya Ugaidi mfano mikoa ya kusini huko
WENGI wao VIJANA hawa hususani wa KIUME ujiingiza katika shughuli hatari ya kuendesha bodaboda, ambapo wengi hupata ajali na kufa au kuumia sana na kupata ulemavu
IKIENDELEA basi hapo miaka ya baadae tutaona kurudi au kuongezeka kwa vikundi vya kiporaji kama panya road na Magaidi watakuepo lakini pia tutarajie kuwa na Tanzania yenye vijana wengi walemavu kutokana na ajali za barabarani😥
Kwa vijana wa KIKE, hawa ndio wanatia sana huruma maana wanakua hawajui cha kufanya na kupatwa na msongo wa mawazo ambapo mwishowe wengi ujikita katika biashara ya kuuza miili yao (kudanga) katika kumbi za starehe, mitaani na kujikita katika ajira hatarishi kama kuuza bar na huduma za masaji na yote ili wapate pesa za kujikimu na kusaidia familia zao ambao nyingi ya familia hizo ni za hali ya chini sana.
IKIENDELEA basi ongezeko la magonjwa ya kuambukiza yataongezeka, watoto wa mitaani na Tanzania yenye (wadangaji) wadada wanaojiuza wengi😓
NINI KIFANYIKE 🙏🏼👇🏽 WITO…
- Mafunzo jinsi ya kuanzisha na kusajili vikundi vya ujasiriamali kisheria na kuchangamkia fursa za vikundi kama mikopo nafuu ya asilimia 10 na zinginezo katika taasisi za kifedha zinazopatikana katika Halmashauri zao.
- Mafunzo ya namna ya kusajili kampuni, uongozi na uendeshaji na masuala ya kodi na leseni za kampuni.
- Mafunzo maalumu ya shughuli kuu za kiuchumi zinazofanyika katika mkoa husika. Mfano Mkoa wa MTWARA na LINDI
(Case Study)…👇🏽
JINSI YA KUFANYA…).
Kwa Sec School (Form 4) …
Liongezeke Somo la lazima kila mkoa ambalo mafundisho yake yatakua yamelenga kutokana na mkoa na fursa zake zikiwemo tekbolojia, masoko, kilimo, uvuvi, ufugaji na wanyamapori… Linaweza itwa SET (Skills for Employment Tanzania).
AU
Baada ya kumaliza mtihani wa Taifa wakati inasubiriwa matokeo VIJANA kwa LAZIMA au HIYARI waendelee kuja shule kwa masomo ya ziada ya kujifunza kujiajiri na kuajiriwa katika shughuli zilizo katika maeneo yanayowazunguka….
Hii inakua kama vile form 6 wanavyokwenda JKT kabla kujiunga chuo.
HITIMISHO….
Tanzania tuitakayo ni yenye kuendelea iliyojaa vijana wenye kudili na Maendeleo na kukuza nchi, familia zao na wao binafsi kiuchumi. Vijana Responsible.
Tanzania ya Matajiri….
Tanzania ya Maboss…
Tanzania ya Wajanja….
Nakupenda Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania 🙏🏼.
Amen.

- Kuwe na mafunzo ya namna ya kulima zao la UFUTA na KOROSHO; jinsi ya kulitunza, kuchakacha, Kupaki, KU brand na kujitangaza mtandaoni. Pia namna ya kuyafikia masoko na kuuza Tanzania na Nje ya Tanzania.
- Kuwe na Mafunzo maalum ya namna zao la UFUTA, KOROSHO linavyo safirishwa na kuuzwa nje ya Nchi hatua kwa hatua kuanzia UBORA (Grade), kununuliwa ghalani, kusafirisha kwa njia ya bandari na masuala ya ushuru na kodi zake.
- Kuwe na mafunzo maalum yanayohusiana na shuguli zote za bandarini (Port Operations) kwenye kuingiza (import? mizigo na kutoa nje ya mipaka (export).