SoC04 Tanzania ya ndoto yangu niitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

joemillimeter

Member
Apr 11, 2015
5
3
Tanzania niitakayo ambayo itatengenezwa na watanzania wenyewe bila kutegemea misaada ya wahisani wenye masharti na vigezo visivyo na ladha ya kitanzania.

1. Tanzania ya wakulima ambao wanalima kwa tija, wakulima ambao watapewa pembejeo za kilimo (mbolea, mbegu bora, mashine za kulimia na kupalilia kwa njia za kisasa dawa za kuulia wadudu) kwa bei nafuu zisizo na masaa au wakapewa huduma hizi bure.

2. Tanzania ambayo viwango vya matajiri na masikini itaondolewa kwa matajiri kuona masikini nao ni watanzania hivyo hawataona ugumu wa kuwainua, masikini kupatiwa huduma za kijamii kama afya, mahitaji ya nyumbani bure.

3. Tanzania ambayo viwango vya ugawaji wa elimu unakuwa ni wa usawa, masikini nao wakasome English medium na viwango vya elimu viwe na usawa.

4. Tanzania ambayo wafanyakazi wa sekta muhimu watakuwa na uhuru wa kufanya kazi zao kwa tija kwa kuwa na malipo yanayowatosheleza bila kuhitaji kufanya mapambano mengine nje ya kazi zao ili kujikimu, walimu, madaktari.

5. Tanzania ambayo viwango vya posho na mishahara ya anasa ya wanasiasa kama wabunge itapunguzwa na pesa hizo zikaelekezwa kwenye sekta muhimu kama sekta ya afya ambapo huduma zote za afya zitatolewa bure.

6. Tanzania ambayo matumizi ya nishati haribifu za mazingira kama kuni na mkaa zitaonekana ni kosa la aibu kutoka mioyoni mwao watanzania, ambapo matumizi ya gesi asilia na gesi kama nishati za kupikia zitapewa kipaumbele.

7. Tanzania ambayo kila mwananchi atajisikia fahari kuwa na nyumba, serikali ijenge nyumba za makazi kwa wananchi wake wote, ili hata wale ambao wanaishi kwenye nyumba za mbavu za mbwa wapate makazi bora.

8. Tanzania ya kijani, upandaji wa miti uwe ni wimbo wa kila mtanzania.

9. Tanzania huruma isiyo na vibaka, wezi, majambazi kwa kuwa ajira zitakuwa nyingi katika sekta nyingi halali kama sekta za usafiri, kilimo, biashara, na sekta za madini.

10. Tanzania yenye viongozi ambao wanachaguliwa na wananchi katika uchaguzi huruma na WA haki, na viongozi ambao watakuwa wanahojiwa Na kutoa majibu bila vitisho pale wanapokosea katika utendaji kazi wao.
 
Back
Top Bottom