SoC04 Tanzania ya Kijani inawezekana, yafuatayo yaweza fanyika katika Sekta ya Mazingira

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ndasika

New Member
Apr 23, 2024
2
3
Tanzania ya Kijani inawezekana
Yafuatayo yaweza fanyika katika Sekta ya Mazingira:
Tanzania ina ukubwa wa takribani Km za mraba 945,087. Ni moja ya nchii liyojaliwa kwa ukubwa ardhi yenye rasilimali nyingi, maliasili na hifadhi nyingi za wanyama, misitu, maziwa na maeneo asili ambayo yote yanaunda Mazingira pamoja na watu wake.

Hata hivyo mazingira haya yaliyokuwa mazuri yameanza kuharibika na kupoteza asilia yake. Hii inatokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na shughuli za Kibinadamu ambazo zinaathiri mazingira. Ikiwa zipo athari zinazosababishwa na Binadamu katika mazingira ni wazi utatuzi wake utatoka kwa watu vilevile.

Kulingana na sense ya watu ya mwaka 2022 Tanzania ilionyesha, kuwa kundi kubwa ni la vijana ambapo ndiyo nguvu kazi ya Taifa la kesho, kundi hili laweza kutumiwa vyema ndani ya kipindi cha miaka kumi na tano hadi ishirini kuibadilisha Tanzania na kuwa ya kijani. NINI KIFANYIKE SASA:

Mosi
, Elimu kwa Umma: Elimu ni nyenzo muhimu katika jambo lolote, hivyo Katika kuboresha Mazingira yafaa kutolewa katika ngazi mbalimbali. Programu za elimu zaweza kuendeshwa shuleni, jamii na Taasisi bila kusahau katika mitandao ya kijamii. Serikali kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zaweza tekeleza jukumu hili kwa kuhakikisha wengi wanatambua umuhimu wa mazingira namna ya kutunza na athari zake kama tutaacha kutunza.


Screenshot_20240527-105139 (1).jpg
Picha mtandaoni, jarida kutoka ofisi ya Makamu Raisi Mazingira

Pili, Kampeni Endelevu za Upandaji Miti: Serikali pamoja na asasi nyingine za Kiraia kushirikiana kwa pamoja katika uhamsishaji wa kupanda miti. Kampeni hizi ziendeshwa kuanzia ngazi ya chini kabisa yaani (Kaya), taasisi zielimu kama shule, vyuo katika ngazi zote pamoja na ngazi ya Kitaifa. Ili kuzaa matunda kwa kampeni hizi, kuwapo na sharia ya kuwapatia miti wanafunzi wanapoanza masomo yao katika kila ngazi.

Mfano pindi mwanafunzi anpoanza Elimu ya msingi apatiwe mti ambao ataotesha katika mazingira ruhusu ya shule na kuutunza kwa kipindi chote cha masomo yake shuleni. Kadhalika na kwa ngazi ya chuo nao wapatiwe miti na kuhakikisha wanaitunza vyema na kukabidhi pale wanapohitimu masomo yao. Katika ngazi ya kaya hali kadhalika wazazi wawapatie maeneo ya kuotesha miti watoto wao walau kila mtoto apande mti wake; katika mazingira yale yanayoruhusu kama maeneo yasiyo ya miji. Kwa upande wa maeneo yaliyo finyu ya mijini baadhi ya miti kama ya vivuli na maua yaweza pia kupandwa kuboresha mazingira.

Tatu, Kuimarisha Usafi wa Mazingira: Uimarishaji wa miundombinu yabkuhifadhi na kuchakata takataka, ni muhimu katika kuhakikisha usafi wa mazingira. Kuanzia ngazi ya majiji na miji hata katika vijiji ni vyema kutengwe maeneo rasmi ya kutupa takataka za aina zote.Mfano taka ngumu,taka laini n.k. Nikitambua maeneo hayo yapo lakini bado hayakidhi uhitaji kwani mengine yamekuwa ndani ya makazi ya watu au miji na hivyo kusababisha adha na uchafuzi wa hali ya hewa. Kumbe yafaa serikali kutumia fursa hiyo kwa kuongeza au kujenga viwanda vyak uchakata baadhi ya taka ambazo zaweza kuwa malighafi kwa matumizi au bidhaa nyingine. Mfano vyuma chakavu na plastiki.

Nne, Matumizi ya Nishati mbadala: Kwa lengo la kulinda na kutunza miti au misitu yetu, ambapo miti imekuwa ikitumika kama chanzo cha nishati kama kuni/mkaa kwa kupikia. Mbadala wa nishati hii waweza kutekelezwa kwa awamu kidogo kidogo hata kupunguza au kumaliza matumizi haya ya kuni. Serikali yaweza anzisha kampeni maalumu kama iliyoendeshwa ya kufukisha umeme katika kila kijiji na kaya kwa bei nafuu;mradi uliojulikana kama (REA). Mbadala huu ni matumizi ya gesi pamoja au uzalishaji wa Biogesi hasa katika taasisi kama shule na kambi mbalimbali. Nishati hizi ni safi na salama kwa mazingira kumbe serikali ifanye kampeni kwa kupunguza na kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa gesi(mitungi) ili walau katika kaya waweze kumudu bei ya matumizi hayo ya gesi. Kampeni hii iendane sambamba na utoaji wa elimu katika matumizi ya nishati hizo.

Kadhalika katika matumizi ya Biogesi, serikali ihamasishe utengenezaji wa miundombinu hiyo katika taasisi zinazotegemea matumizi ya kuni katika kupika, hii ni pamoja na kuhakikisha kutunga sheria ya matumizi ya biogesi katika taasisi zenye mazingira yote wezeshi ya kujenga miundombinu hiyo.

Tano, Matumizi sahihi ya ardhi na vyanzo vya maji: Elimu ni muhimu kabla ya kuweka sheria za kufuata, ikiwa asilimia kubwa ya Watanzania wanajihusisha na kilimo pamoja na shughuli nyingine zinazohitaji ardhi; elimu yafaa kutolewa. Kwani matumizi yasiyo mazuri ardhi kama utumiaji wa kemikali zinazoondoa rutuba ya udongo, uchomaji wa misitu na utelekezaji wa ardhi yote huathiri mazingira. Kumbe maafisa ardhi katika ngazi zote wanahitajika ili kuweza kudhibiti matumizi hayo yasiyo sahihi, na kuonyesha l namna nzuri ya kutumia ardhi.

Sambamba na matumizi hayo ya ardhi, utunzaji wa vyanzo vya maji ni muhimu, mbali na elimu serikali iboreshe upatikanaji wa maji safi kwa wananchi ili kusaidia kuzuia, kwenda kufuata huduma ya maji katika vyanzo vyake, pia kwa wakulima wakubwa na wadogo kuwepo na mfumo rasmi wa umwagiliaji wa mazao yao Mfano matumizi ya mabwawa na pumpu katika kusambaza maji. Vilevile kwa wafugaji wanaopeleka mifugo kupata maji katika vyanzo vya maji ni vyema wakawa na umoja kuanzisha ranchi au kujenga majoshi kwa ajili ya kuogesha na kunywesha mifugo yao. Hii itasaidia kupunguza au kumaliza tatizo la watu kufanya shughuli
zao katika vyanzo vya maji.


Screenshot_20240527-105049 (1).jpg

picha kutoka mtandaoni

Hitimisho, utunzaji wa mazingira unatuhusu sote kumbe serikali itafanikiwa kwa yote hayo kwa ushirikiano wa wananchi. Ni jukumu la kila mmoja kupenda na kutunza mazingira kwani ndiyo yanayotupatia mahitaji yetu.

Chapisho na Julius Ndasika
 
Mfano pindi mwanafunzi anpoanza Elimu ya msingi apatiwe mti ambao ataotesha katika mazingira ruhusu ya shule na kuutunza kwa kipindi chote cha masomo yake shuleni. Kadhalika na kwa ngazi ya chuo nao wapatiwe miti na kuhakikisha wanaitunza vyema na kukabidhi pale wanapohitimu masomo yao. Katika ngazi ya kaya hali kadhalika wazazi wawapatie maeneo ya kuotesha miti watoto wao walau kila mtoto apande mti wake; katika mazingira yale yanayoruhusu kama maeneo yasiyo ya miji. Kwa upande wa maeneo yaliyo finyu ya mijini baadhi ya miti kama ya vivuli na maua yaweza pia kupandwa kuboresha mazingira.
Nzuri.

na matumizi hayo ya ardhi, utunzaji wa vyanzo vya maji ni muhimu, mbali na elimu serikali iboreshe upatikanaji wa maji safi kwa wananchi ili kusaidia kuzuia, kwenda kufuata huduma ya maji katika vyanzo vyake
Sawa sawia, elimunni muhimu
 
Back
Top Bottom