Tanzania tunahitaji kila mmoja kujitafakari na kujua atasaidiaje kulikomboa taifa

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Jana wakati naangalia Taarifa ya habari niliona wabunge wakihoji ni lini serikali itapeleka mikataba bungeni.

nilijiuliza mengi nikajiuliza hivi kuipeleka mikataba bungeni tutatatua matatizo ya mikataba?

ni rahisi sana kuona kama naunga mkono serikali lakini jifanye kama hujui ninaipinga au naiunga mkono unisikilize kwanza uelewe ninallolisema alafau ndio ulihukumu.

kwangu mimi ninaona tanzania ikiwa tunachukulia mambo kirahisi na kila mmoja akijaribu kutafuta ugali wake huku akidai matatizo tuliyonayo ni kwa yeye kutoshirikishwa. hivi kweli hili ndilo tatizo letu?

kwanza kabisa najiuliza ni mambo mangapi yamepita bungeni na bado yanatoka huko mambo ni yaleyale. nakumbuka kuna wakati niliwahi kusikia waziri akiliambia bunge kuwa alienda kusaini mkataba wa madini ulaya kwa kuwa tungepoteza kiasi fulani cha fedha na bunge lilikubaliana na waziri huyo.

niliwahi kuandika katika mtandao huu wa kijamii kuwa bunge letu ndio mzigo namba moja. mimi ninaamini kama bunge lingekuwa makini kwa majukumu waliyopewa ya kusiamamia na kushauri serikali tusingekuwa na serikali zinazofanya vibaya.

lakini kama msimamizi mwenyewe hajui wajibu wake na hatimizi maana hawezi kutimiza asilolijua unategemea serikali ifanye nini kama sio bahati nasibu, ikifanya vizuri haya aikifanya vibaya haya.

kwanza huwezi kufanya kazi ya kusiamia na kushauri bila utaalamu, sasa bunge utaalamu linaupate?

tujikite katika swala la mikataba hii, hivi bunge lina utaalamu gani wa kupitia mikata kama sio watu kutumia madaraka tuliyowapa badala ya kuweka utaratibu mzuri bali wanataka kujilundikia kila kitu na mambo wasiyaweza na kufanya ubabaishaji ndani unaoligahrimu taifa.

tatizo linalotuingiza katika mikataba mibovu ni nini? je ni corruption? je ni utaalamu wa watu kujua mbinu na vigezo vya kimikataba ili kulitetea taifa na kuweka vipengele vizuri katika mikataba?

hivi wengi wetu tumekuwa tukisikiliza bunge, mtu anasimama kuchangia hoja muhimu anachokifanya ni kutaja majina ya vijiji na kata kwenye jimbo lake na huyo ndiye anayepigiwa makofi na wabunge wenzake. hivi tunadhani tunaweza kuondoa mikataba mibovu kwa kusema tuipitishe bungeni? hawa wana utaalamu gani?

sasa kama ushauri wenyewe unaotolewa na bunge juu ya mikataba ndio huo wa kutaka wao ambao wanaunda kamati ambazo upo uwezekano wa kukuta mwaka fulani kuna taaluma haikuingia bungeni kutokana na wanaoingia wanatumia vigezo tofauti. watafika huko wataunda kamati mfano kamati imejaa walimu tu eti inaletewa mkataba wa madini kuupitia na wanaona wakiipitia wao ndio kutaondoa tatizo la mikataba mibovu?

hoja yangu ni hili tatizo haliko kwa bunge tu, sote katika jamii hatukai kujitafakari na kuangalia kila wetu mimi kama mimi au sisi kama sisi wajibu wetu katika taifa hili ni upi.

sote tunabaki kutazama wengine na kudhani tukichukua majukumu ya wengine ndio mambo yatakwenda vizuri. hivi kwa kufikiri hivyo je tunakuwa sahihi au bado tunaendeleza ubabaishaji?
 
Kulikomboa taifa ki vipi? Maana Mkapa alitoa povu sana wakati wa kampeni na kuita watu wapumbavu na malofa, kwa kuwa "NCHI ILISHA KOMBOLEWA" .
 
maneno kuntu haya, nashangaa watu wanavyoshabikia siasa na kubishana hapa, badala ya kufanya kazi na kujiongezea maarifa zaidi,
kuna nchi zina uongozi mbaya na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu lakini wanafanya kazi na wana maendeleo makubwa

watu wanashabikia siasa, mpira, wasanii, wanasoma wanatarajia kukaa ofisini, yaani hakuna creativity yoyote, huku wachina, wakenya wakija kuchukua fursa huku tz, nchi inakuwa flooded na bidhaa za nje na wataalamu kutoka nje
hii ni aibu wajameni
 
Yupo mtaliano mmoja alikuja bongo hana kitu leo hii ni mmoja wa viongozi wa chama cha wasafirishaji mizigo Tanzania. Anaitwa Massimo, aliinuka kidogo kidogo, sasa hivi ni tajiri mkubwa. Fursa alizoziona sisi wengine wala hatukujisumbua kuzihangaikia. Tunachoweza ni kukosoa kila kinachofanywa hatuna hata wazo jingine mbadala ambalo ni bora kuliko hata kile tunachokikosoa.
 
hii inasikitisha kwa kweli kuna mchina eti yupo ana supply maji ya kunywa watanzania wamekaa tu, biashara wakianzisha ni zile zile za baa na gesti, na ku supply bidhaa yaani hakuna ubunifu kabisa
 
Aibu ya Nani? Biashara za maandazi na vitumbua lazima zife. Wanaotegemea kuuza ice cream na visheti imekula kwao. Chai itakuwa luxury. Kwa kifupi sukari imepotea. Sasa wekeni bei elekezi kwenye asali. Sh 7000 kwa kilo hatutaweza.

Nchi haina DIRA! Inaangalia leo kesho itajijua yenyewe. Siku hizi ni kujilinda tu na kujiandaa kutumbuliwa. Kama sio na Magufuli basi hata yule trafiki. Hujui eneo unalokaa ni halali, hujui kama kibanda chako utamaliza, hujui Kama mikopo uliyochukua utaweza kurudisha maana wateja wamekimbia. Hujui kama trafiki atakupa tiketi kwa vile gari lako chakavu.

Mh. Rais kuna maisha zaidi ya majipu. Usitusahau sisi ambao hatukufisadi. Tuliadhibiwa na mafisadi na wewe sasa unanyunyiza chumvi kwenye vidonda vyetu.

Na ni bora tujadili siasa na mpira la sivyo idadi ya watanzania lazima itaongezeka kwa kiwango kikubwa mwaka huu (katika kutafuta faraja).
 
hii inasikitisha kwa kweli kuna mchina eti yupo ana supply maji ya kunywa watanzania wamekaa tu, biashara wakianzisha ni zile zile za baa na gesti, na ku supply bidhaa yaani hakuna ubunifu kabisa
Na kwenye hizo biashara za Bar wanaishia kutembea na ma-barmaid, wanaishia kuupata au kuueneza ukimwi. Halafu kero nyingine ni kwamba tunaridhika na mambo madogo sana.
 
Kwa hiyo bei ya sukari ndio imeua fursa zote? changamoto zipo ndio lakini as individual kuna njia za ku beat hizo changamoto na kusonga mbele, ukikaa ukijadili madhaifu ya serikali kila siku bila kujadili mbinu za kukabiliana na changamoto zinazotokana na madhaifu hayo utaishia kuwa mlalamishi tu na kufa masikini
 
Na kwenye hizo biashara za Bar wanaishia kutembea na ma-barmaid, wanaishia kuupata au kuueneza ukimwi. Halafu kero nyingine ni kwamba tunaridhika na mambo madogo sana.
Nashangaa sana watanzania wamekaa kujadili changamoto za system ya utawala na kuishia kulaumu, lakini hawajadili namna ya kukabiliana na hizo changamoto wanakaa na kuishia kulaumu tu, mimi nawaasa sana wanangu usiilaumu system kwa kukufanya ushindwe kutimiza mipango yako, jilaumu wewe kwa kushindwa ku beat changamoto za system kutimiza maleng yako
 
mengine yanasababishwa na hv vya siasa havina system ya kuandaa viongozi wao ikifika wakati wa uchaguzi wanachukua watu wanaoona watapata kura nying af wale viongoz wazuri wanawaacha matokeo yake ndio hayo
 
Hivyo hujui sukari haiko mitaani? Maamuzi ambayo yalifanywa na viongozi wenyewe licha ya ushauri waliopewa. Naona mpika maandazi na vitumbua ni mtu mdogo sana kwako, huyu mama analisha familia na hizo pesa kidogo anazopata. Sina takwimu lakini najua hawa wamama wako wengi Tanzania. Serikali ina wasomi na lazima tukubaliane hapa watanzania wengi hawako vizuri kielimu, wanahitaji mwongozo wa viongozi wao. Unachotaka huyu huyu mlalahoi ambaye hajui hata Leo usiku atakula nini na watoto afikirie mbinu mpya? Mwogopeni Mungu jamani! Ukiwa nacho usifikirie mwenzako hataki au mvivu, hajui hata pa kuanzia.

Mungu ibariki nchi hii! Umetutoa kwenye one extreme sasa unatutupa upande wa pili kabisa!
 
mengine yanasababishwa na hv vya siasa havina system ya kuandaa viongozi wao ikifika wakati wa uchaguzi wanachukua watu wanaoona watapata kura nying af wale viongoz wazuri wanawaacha matokeo yake ndio hayo

nadhani tatizo ni mfumo tulio uweka kwenye katiba.

tumeunda bunge kikatiba kwa kuangalia dhana ya uwakilishi wa wananchi bila kuangalia majukumu tunayolipa bunge kuwa yanahitaji kutumia utaalamu pia.

kwa jinsi gani tunaweza kubalansi haya mawili?

nadhani ingekuwa busara mfano hawa wajitambue kuwa nao hawana uwezo wa kupitia mikataba na kuishauri serikali mfano kusema mikataba ipitiwe na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na hawa waunde kitengo maalumu cha kupitia mikataba tena kabla haijasainiwa.

vyama vya siasa vyenyewe vinajali kuweka mgombea atakayeshinda sasa nani asimamishe mtaalamu kwenda bungeni kama kuna mtu ni popular anaweza kupata kura hata kama hana ujuzi wa kusiamia serikali?
 
Kulikomboa taifa ki vipi? Maana Mkapa alitoa povu sana wakati wa kampeni na kuita watu wapumbavu na malofa, kwa kuwa "NCHI ILISHA KOMBOLEWA" .

hatuwezi kulikomboa taifa kwa ushabiki wa vyama, na nikiuleze mtu yoyote anayetaka maendeleo haingii kwenye ushabiki wa vyama kama mpira.

tukisema kulikomboa taifa tunaongelea kupunguza umasikini, tunaongelea kuongeza huduma za jamii, tunaomngelea mambo ya maendeleo ya watanzania.

sasa unaona hatuhitaji kufikiri kila mmoja wetu tumepeana majukumu gani au kila mmoja ana mchango gani kwa kuwa fulani alisema hivi wakati fulani.

kumbuka mwalimu aliwahi kusema yapo mambo mazuri waliyafanya na yapo mabaya waliyafanya akashauri tuchukue yale mazuri tu ili yatusaidia na mabaya tuyaache.

hivyo mtu yoyote ambaye alitupa jambo la kutusaidia tulichukue litusaidie na la kipuuzi tuachane nalo.
 
na wakipata nafasi hua wanaongea kweeeli kwa mbwembwe utadhan wana utalaamu
 

sina uhakika kama unalolisema linawezekana!

hivi unajua system ina mchango gani katika maisha ya mmoja mmoja?

kwa taarifa yako system ni kama unavyoona mtandao wa simu za mkononi katika mawasiliano ya simu. kama mtandao haupo mtu mmoja mmoja anawezaje eti kujiangalia yeye?

mpaka mtandao uwepo unaofanya huduma kuwepo na ndipo mtu mmoja mmoja anaweza kununua simu, kuweka vocha na kutumia.

bila system kufanya kazi mtu mmoja mmoja hakuna analoweza kufanya maana system ipo kurahisisha upatikana wa mambo yanayotoa fursa kwa jamii na hapo ndipo mwanajamii mmoja mmoja anatumia fursa.

mfano tuongelee mikataba ya madini. niambie mtu mmoja mmoja afanye nini?

lakini jukumu hili tumewakabidhi serikali kutumia madini haya na sisi huku tupate fedha za kigeni kununua vitu kutoka nje na vitu hivi vikija kwetu vinatoa huduma na ajira.

serikali inaonekana kuzembea lakini sisi tulishajua kuwa hakuna anayeweza kufanya kazi bila kusimamiwa akafanya vizuri bali kuna uwezekano wa kuacha kumtumikia mwajiri wake na kuigeuza ofisi yake. tukaunda bunge ili likasimamie sasa bunge linatoa ushauri wa kama serikali inafanya blanda basi kazi hiyo wailete kwao. sasa sijui kama uliwaza ulilolisema kuwa kila mmoja atafakari kivyake badala ya kukaa kama jamii tukajiuliza hivi hawa tuliowatuma kuna tatizo gani?

yaani ni sawa umeweka mtu katika biashara zako anatakiwa kuwa na utaalamu wa biashara na mahesabu kuendesha biashara zako na ukampa ndugu yako madaraka ya kuwasimamia watendaji. sasa alipewa kazi tena akiwa ana utaalamu au akitakiwa na utaalamu mahesabu yanaonekana kuleta hasara, eti ndugu yako huyu alitoka kijijini anasema mahesabu aletewe akague yeye hivi kweli huyu anajua tatizo na anaweza kulitatua? hoja yangu hapo ni tulitegemea ndugu huyu kutambua umuhimu wa utaalamu katika kazi hiyo na kujua upo uwezekano wa huyu aliyepewa kazi hatumii utalamu na ushauri sahihi ni kutafuta mtaalamu wa kupitia mahesabu haya na kubaini tatizo liko wapi.

kusema watu wanalamika tu na kutaka wakuletee majibu ni kuonyesha tabia ya uzembe! mtu ameona tatizo na tatizo hili linahusu jamii nzima anatakiwa alilete kwenye jamii, kwanza jamii nzima ione tatizo lenyewe na jamii nzima ishiriki kila mmoja kutoa mchango wake ni jinsi gani tatizo linaweza kutatuliwa.

n
 
hii inasikitisha kwa kweli kuna mchina eti yupo ana supply maji ya kunywa watanzania wamekaa tu, biashara wakianzisha ni zile zile za baa na gesti, na ku supply bidhaa yaani hakuna ubunifu kabisa

kuna mambo sio kosa la watanzania.

akili ya mwanadamu inategemea mazingira yaliyomzunguka hivyo mtu alitoka katika jamii zilizopiga hatua ni rahisi sana kuona fursa nyingi za ajira akienda katika jamii ambayo haijapiga hatua kuliko mtu aliyetoka katika jamii iliyo chini akienda katika jamii iliyopiga hatua.

mfano dar kuna watanzania wanatoka vijijini na kuna wenzetu wanatoka ng'ambo. wa kutoka kijini akienda mjini fikra zake zote zinawaza mihogo, viazi na kadhalika mambo aliyoazoea lakini yule wa kutoka nje anawaza mambo aliyaona huko kwao.

hivyo huyu aliyetoka nje ni rahisi kuanzisha huduma alizoziona kwao katika jamii aliyokuta huduma hizo hazipo, ana uzoefu wa jinsi gani ya kupata mtaji kwa uzoefu wa kutoka kwao.

huyu wa kijini kwanza haamini kama anaweza kufanya jambo lolote bila kutumia fedha yake mfano kutumia mkopo.

hapa ndipo tunarudi kwenye system kuwa ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya watu.

serikali zetu zipo kutambua jambo hili na kufanya tafiti kujua ni huduma gani zinaweza kuwa tija katika jamii, kuwapa elimu hawa waliotoka vijijini ili kuondoa miogo na viazi katika fikra zao, kuwapatia mitaji, kuwalinda kimasoko maana huwezi kutoka kuchoma mihogo ukaja kutengeneza ice cream ikashinda na ya yule wa nje mwenye uzoefu wa kutengeneza ice cream kwa miaka mingi bila shaka ice cream ya mtu wa kijijini itakuwa imeungua hata kama ni ice.

hivyo kama system haifanyi kazi watu hawa wa vijijini wataendelea kuwaza mihogo na viazi wakati mjini mihogo na viazi havina dili huku watu wa nje wakipiga maisha.

kibaya zaidi ni pale wale waliotakiwa kuwaongoza wanapokuwa nao wanawaza mihogo na viazi na kutaka kuwalazamisha kurudi kujijini bila kujua kama walioko kijijini kwa sasa maisha yao ni hohehahe, na hawa wamekimbia huko kuja kutafuta maisha bora je kuwarudisha kwa nguvu ni kuwakomboa au ni kutumia nguvu kuwarudisha katika maisha ya dhiki?
 
Umeandika maneno mengi lakini hoja ni neno KUKOMBOA, haijalishi kichama aua kibinfsi, hilo neno ndio lililo kataliwa na kuambiwa nchi imesha kombolewa, litafutwe neno lingine badala ya hilo.
 
Umeandika maneno mengi lakini hoja ni neno KUKOMBOA, haijalishi kichama aua kibinfsi, hilo neno ndio lililo kataliwa na kuambiwa nchi imesha kombolewa, litafutwe neno lingine badala ya hilo.

usinipereke huko maana naweza kuiondoa mada kwenye mstari. labda in soti mimi naweza kusema sikubaliani na wote waliokuwa wakipingana katika hoja hiyo kwa waliyoyasema. maana alilolisema mkapa kuwa nchi imekwisha kombolewa silikubali kwa maana uhuru wa mwanadamu uko shakani wakati wote. maana ya uhuru kwa mwananchi ni kujichagulia viongozi ni kwa kuandika jina kwenye karatasi bali kuwa na uelewa wa maana ya kiongozi na kuchagua mtu wa kufanya kile kiongozi anachotakiwa kufanya kwa waliomchagua na pili kuwa na udhubiti wa rasilimali zao. hapa unaweza kuona wanadamu hasa wa nchi za dunia ya tatu wanahama kutoka kwa mkoloni huyu na kutoka kwa mkoloni huyu na kuhamia kwa huyu. yaani kama mtu anachagua kiongozi kwa kutumia rushwa huyu hajui maana ya kiongozi na hayuko huru haijalishi amepiga kura. pili kama mwananchi huyu hana udhibiti wa rasilimali zake basi huyu hayuko huru haijalishi anasherekea uhuru kila mwaka.

nikirudi upande wa pili ninweza sikubaliani na hoja waliyokuwa wakiitoa kwani ninweza kuwaeleza kwa wimbo wa "pro J" kuwa wanahubiri amani huku wameficha mapanga mifukoni. tatizo kubwa la uhuru wa mwananchi ni ujinga wa mwananchi kutotambua maana ya uongozi. bado naona maneno yaliyotumika kutake advantage ya ujinga wa wananchi kama misemo ya nyerere, nyimbo za ukombozi za afrika kusini lakini nchi hii imejikwaa wapi nilkuwa nikiwaona wameyakumbatia zaidi kuliko wanavyoyapinga majukwaani. anyway kinachotokea kwa sasa kinaweza kuwa ni ushahidi na tunaweza kujiuliza hivi wangeshinda wangefanya haya? lakini waliyokuwa wakisema yalimaanisha haya ndio maana nikasema niliwaona wameficha mapanga mifukoni huku wakihubiri amani.

ukombozi ulioko hapa si porojo za kutafuta madaraka ya kisiasa bali ni kusema tutajikomboa kama kila mmoja wetu akitambua kwa nafasi yake yeye aliyonayo mchango wake ni upi na je anatimiza na kama kuna mapungufu je afanye nini kuboresha.
 
there is always a way,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…