Tanzania tulijenge bomba! Kenya wabaki wanashangaa

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,598
SISI WATANZANIA LAZIMA TUZIINUE SAUTI ZETU NA KUKATAA MTANDAO UNAOZUSHA KUWA TANZANIA HAIWEZI KUJENGA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA KUJA BANDARI YA TANGA.

Mimi naanza kwa njia ya SHAIRI hapa chini;
1. Watanzania tuko bomba, kulijenga hilo bomba, acheni kutusumbua, mwishowe tukawatumbua, hapa kwetu kazi tu hatutaki zenu ndumba, na kamwe hatutayumba, kuitetea nchi yetu bomba, mafuta yatalipita bomba, hadi Tanga tutayasomba, watanzania tuko bomba, tutalijenga hilo bomba.

2. Bongo zetu ni spesho, wala sio za mitumba, ngojeni ikifika kesho, hakika tutalijenga bomba, hata mkileta ndumba, kwa sasa hatutayumba, watanzania tuko bomba, kesho tutalijenga bomba.

3. Kwa kutumia tafiti, TANGA ni njia rahisi, LAMU tukafate nini?, acheni hoja mfu, ati hatuna uzoefu, mbona tulijenga TAZAMA na Gesi ya mtwara mpaka Dar,wataalamu kedekede tunao, waliojawa uzalendo, tutalijenga bomba kwa kishindo, liwe kwetu ajira na lindo, ajira tumezisikia, za kudumu 1500, za muda zaidi ya 5000, watanzania tuko bomba, ukweli mmelikosa bomba.

4. Acheni propaganda, kuihadaa uganda, Tanzania kuiponda, ati hatuwezi kulijenga!, tena muache kabisa, kuja kwetu kwa kujificha, kule Tanga mmekamatwa, kwa aibu leo(24/3/2016) mchana kweupe, jueni tuko bomba, hakika tutalijenga bomba.
 
Bomba halijengwi na
Uganda,TANZANIA, wala Kenya
Bomba linajengwa na Total
Kenya na Tanzania ni njiatu
Mwamuzi wapinjia ya kulijenga ni Mganda

Tunacho paswa Watanzania nikukomaa kukabana na Mkenya kumtongoza Mganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…