Tanzania tulichelewa kumpata rais kama Dr Magufuli

jaruri

JF-Expert Member
Jul 16, 2014
717
459
Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuamini maneno na kauli za baadhi yetu ,na unaweza jiuliza kuwa ni watanzania kweli ? Au wanatumiwa na watu Wa nje wasio tutakia mema,,,

Naweza toa mfano mmoja Jana nimetoa post hii akaja MTU mmoja kwa sababu binafsi akanipinga kwa ku-refer cartoon ya Kenyan cartoonist Gado akidai Rais kavunja katiba kama vile haitoshi aka edit post yangu kwa kuweka hiyo cartoon ya GADO,,najiuliza moderator haoni au hawa watu wana lengo gani ?
Kama ni mtanzania MWENYE akili timamu huwezi copy cartoon ya MTU Wa nje na wewe bila kutafakari ukaichukua kama ilivyo then una comment kuwa Rais kavunja katiba how? Mkenya ndo anaijua katiba yetu kuliko sisi? Narudia wito WANGU kwa watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na nchi yetu tuitumie mitandao ya kijamii vizuri kwa faida ya taifa letu na tupinge na kukemea kwa nguvu zetu zote post zote zenye viashiria vya uchochezi,,,,
Long live JPM; Hapa kazi tu.
 
Nakazia
 
Jaruri ndugu kuna mada zingine ukiweka ktk mitandao tegemea kupata opponents wengi sana.

Kila kitu na muda wake kwa sasa watu wengi wana hasira na Rais Magufuli kwasababu tofauti.

Usishangae kupata huo upinzani hata kwa cartoons ya Kenya tu.Hata wanajua kuwa Rais Magufuli Anafanya mambo mengi mazuri kwa wanainchi wake lakini kuna watu wanajenga ngome kuwa si kweli.

Kwasababu Dr Magufuli ameanzisha vita ya kimaslahi kwanza,kutumbua majibu,madawa ya kulevya,wafanyakazi hewa,wanafunzi hewa,makontena hewa,udhibiti wa kodi kila mahali.kila Mbunge afanye mikutano kwenye Jimbo lake.

Kwa hayo na mengine mengi ni vita hiyo usitegee usemwe vizuri hata kama unafanya vizuri.

Ila kiuhalisia ameliokoa taifa na uharamia mkubwa sana uliokuwa unaendelea.
 

Bashite je?, mbona anamwacha!
 
Ajira ziko wapi alidai ataongeza ajira ndo hivi sasa tunaishi kwa kuangalia vyama tusijiendekeze Tanzania kwanza Raisi asiye jua matatizo ya wananchi wake , nashangas sana unakuja kusema hivi kwani umesha jiuliza ni nchi gani serikali inatoa mokopo kwa wanafunzi baadae ina katisha mikopo hiyo ndo nimeona Tanzania nchi ambayo watu wachache wana thamani kuliko watanzania wote mishahara toka isimame kupanda ni miez mingap hadi sasa bado Hamna chochote nchi inayo toa taarifa za uongo eti tumekusanya kias flani huku hatuoni hizo hela zikifanya kaz gan ameahid atajenga mahakama ya mafisadi hadi Leo hamna fisadi yoyote aliye fungwa nchi ambayo kujuana kumejaaa ni Tanzania pekee ambayo viongoz wanatafuta kuonekana kwenye vyombo vya habari nasema kwakuwa ukitaka kujua hali ya hii nchi usitake kuegemea we we wa chama gani simama katikati to a ukweli tusipambe vitu kwa manufaa yetu
 
Kikwete alikuwa mpole watu wakamuita rais dhaifu tena hapa hapa kwenye hili jukwaa,Magufuli kawa mkali,watu wanalalama eti kazidi ukali hata kudiriki kumkumbuka Kikwete(tuliona hivi karibuni Wabunge wakiwemo wa upinzani waliokuwa wanamnanga)Sasa Watanzania tunataka rais wa aina gani?
 
kwa madai yao wanamtaka Lowasa
 
Ajira hazioti kama uyoga zinatengenezwa na rais anatengeneza nafasi za ajira kwa kuhimiza uwekezaji mbalimbali katika sekta kama viwanda utalii na biashara,,ni juzi tu hapa kwenye uzinduzi Wa ujenzi Wa reli katangaza kuwa waajiriwe watanzania kwa asilimia kubwa,,haya waalimu tayari washatangaziwa ajira na ajira zingine zinakuja,,mambo yanaenda kwa mipango na taratibu.Na kwa taarifa yako hakuna nchi inayo ajiri wahitimu Wa Chuo kikuu kwa asilimia mia moja lazima kuna wanao kosa ajira serikalini na hivyo hujiajiri wenyewe au huajiriwa kwenye sekta binafsi,,ni juzi tu hapa tumesikia kuna madaktari 1500 Kenya hawana ajira hivyo sidhani issue ya ajira ni hoja unayoweza kuileta kuilaumu serikali ,,zingatia mikakati ya serikali katika kuongeza fursa za ajira nilizo ziainisha hapo juu!!
 
Atakuwa anawatuma sio bure kupima upepo.ebu fikiria ile tweet ya reli.ingemsema vibaya magufuli wangepona?
Hawa watoto wa Lumumba ni vichaa kabisa makampuni yanafungwa watu hawana ajira watoto wa vyuo wanamaliza vyuo pa kwenda hawana sembe 2000 sukari 2400 sasa hata sisi masikini tulikuwa wapiga deal kweli?.hawa watoto wa Lumumba kiama watakuwa kuni
 
Hawa watoto wa Lumumba ni vichaa kabisa makampuni yanafungwa watu hawana ajira watoto wa vyuo wanamaliza vyuo pa kwenda hawana sembe 2000 sukari 2400 sasa hata sisi masikini tulikuwa wapiga deal kweli?.hawa watoto wa Lumumba kiama watakuwa kuni
Hawa nao ni majipu.wakamwambie aliyewatuma kwamba watu wanatamani hata apunguziwe muda.tuitishe uchaguzi
 
Kwanza Magu ni kiongozi mzuri kabisa, sio kwamba hajafanya kitu; kuna vingi tu vizuri amevifanya. Hata hivyo yeye sio Malaika. Kuna udhaifu mwingi tu pia ameuonesha. Hatuwezi kusema tumsifie tu kwa mema aliyoyafanya na tusahau kuwa kuna mabaya au madhaifu aliyoyaonesha, hapana.

Tunachopaswa kufanya ni ku'acknowledge aliyoyafanya vizuri na kum'criticize kwa udhaifu aliouonesha. Hata yeye anapaswa kuelewa na kuwa tayari kupokea criticism na kuchukua hatua.

Otherwise, tutakuwa hatumsaidii yeye na Taifa kwa kuleta ushabiki usiokuwa na kichwa wala miguu. Point yangu ni kuwa anapofanya mema asifiwe na anapofanya vibaya aambiwe pia. Tuitangulize Tanzania mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…