SoC04 TANZANIA TUITAKAYO: Wizara ya Elimu, maendeleo ya Sayansi na teknolojia

Tanzania Tuitakayo competition threads

Paramountrose

New Member
Jun 30, 2024
2
2
Stories of change.

Maoni yangu kuhusu Tanzania tuitakayo, napenda kuyaelekeza kwa kiasi kikubwa katika Wizara ya Elimu, maendeleo ya Sayansi na teknolojia. Katika kuiboresha Wizara hii naishauri sana Serikali isielekeze nguvu zake zote kwenye Shule za Sekondari, Vyuo vya Kati na hata Vyuo Vikuu bali Serikali iwekeze nguvu zake nyingi katika kuiboresha Elimu ya Msingi kwasababu hapo ndipo tunapomtengeneza mtoto awe vile ambavyo wazazi, Taifa na hata Serikali inavyotaka mtoto awe kwasababu katika umri huu mtoto anaweza kuelewa na kukariri vitu kwa haraka.

Nitoe wito kwa Serikali kufanya maboresho kwenye Elimu ya Msingi kwa kuwaajiri walimu wa kutosha hasa walimu wa somo la kiingereza ambao watafanya Kazi kwa moyo wao wote, kwa nguvu zao zote na kwa akili zao zote.

Watoto wa shule ya msingi wanatakiwa kupikwa haswa kabla hawajafika Sekondari. Wanafunzi wanatakiwa kujua kuzungumza lugha ya kiingereza vizuri wakiwa shule ya msingi kwasababu masomo yote katika shule za Sekondari yanafundishwa kwa lugha ya kiingereza isipokuwa somo la Kiswahili na somo ambalo linahusu lugha ambazo zinazungumzwa nchi nyingine ikiwemo Kifaransa na kichina Wanafunzi wanaripoti kidato cha kwanza wakiwa hawaelewi kabisa lugha ya kiingereza wanajikuta wakiwa kwenye wakati mgumu na kushindwa kuelewa masomo kwa wakati.

Shule za msingi za Serikali zinaweza kuwatengeneza wanafunzi wa shule hizo zikawa kama shule za English medium. Serikali inatakiwa kubuni mikakati ambayo itawafanya walimu wafanye Kazi kwa kujitoa hii ni maana halisi ya kusema kuwa ualimu ni wito. Kama watoto wataripoti kidato cha kwanza wakiwa wanaweza kuzungumza, kuandika na kusoma lugha ya Kiingereza. Wanafunzi hawa watapenda shule, watakuwa wanajiamini na watajituma.

Naipongeza Serikali kwa kuubadilisha mtaala wa Elimu kwasababu hivi sasa wanafunzi watajifunza ujuzi wa aina mbalimbali wawapo shuleni hii itamsaidia mwanafunzi pia kutambua kwa haraka kitu anachokipenda na kujiendeleza kielimu kuhusu ujuzi huo. Jambo ambalo litasaidia pia kumpa uelewa muhitimu pale atakapohitimu masomo yake aweze kujiajiri na sio kusubiri ajira kutoka kwenye Serikali na makampuni binafsi.
Naishauri Wizara ya Elimu pia ianzishe program yoyote kwaajili ya kuwasaidia wahitimu ambao walimaliza masomo yao wakati ambao tulikuwa tunatumia mitaala ambayo ilikuwa haimuandai muhitimu kujiajiri, vijana wengi wameathirika kisaikolojia hawajui kwasasa wafanye nini ili wawe na maisha mazuri au wapate kipato ili waweze kulea familia zao na kutuliza majukumu yao kwa jamii na hata Taifa. Vijana wamekuwa na majuto kwanini hivi kwanini sina ajira kwanini maisha yapo namna hii. Wizara inatakiwa kutafuta namna ya kuwapa wahitimu hao ujuzi mbalimbali ili waweze kujiajiri na sio kuendelea kusubiri ajira.

Wizara ya Elimu ihakikishe shuleni vinapatikana vifaa vya kufundishia mfano vitabu ili wanafunzi wasisome kwa nadharia. Wawe wanasoma kitu ambacho wanakiona hii itasaidia sana kuvuta uelewa wa mwanafunzi na kufanya mtoto aweze kuelewa na kukumbuka kwa haraka. Hivyo Serikali inapotaka kufanya mabadiliko yoyote kwenye Elimu inapaswa kuhakikisha imeandaa vitabu vya kutosha na mazingira rafiki ambayo yanaendana na mabadiliko hayo.

Serikali imuwezeshe mwalimu ili aweze kufundisha kidigitali na aweze kuendana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia mfano kompyuta, vishikwambi, vipaza sauti nk hii itasaidia kufanya watoto wavutiwe na mazingira ya shule na kupenda kumsikiliza mwalimu na kujisomea kwasababu mazingira yanahamasisha watoto kusoma.

Serikali iboreshe elimu ya awali kwa kununua vifaa mbalimbali ambavyo vitamvutia mtoto kupenda kwenda shule. Kuna vifaa na picha mbalimbali ambazo zinaweza kutumika wakati wa kufundishia na kwenye michezo ya watoto . Vifaa hivyo vinapatikana sana katika shule za Taasisi na watu binafsi pekee hii inachochea wazazi wengi kuwapeleka watoto wao katika shule za watu binafsi na sio shule za Umma kwasababu mazingira ya shule za Umma sio rafiki kwa watoto. Walimu wapewe elimu pia juu ya umuhimu wa kutengeneza zana za kufundishia na kuzibandika darasani kwasababu zana hizo zinapendezesha darasa na kuvuta uelewa pamoja na kumbukumbu za mwanafunzi.

Naishauri Serikali kama idadi ya wahitimu katika kada fulani ni wengi na Serikali haiwezi kuwaajiri hao watu kwa wakati, Serikali iamue kusitisha idadi ya wanafunzi kuendelea kusoma kozi hiyo na kutunga Sera ya muda ambayo itawaelekeza wahitimu wa kidato cha nne na cha sita kusoma kozi nyingine ambazo zinahitajika kwasasa. Hakuna nchi ambayo imeweza kuwapa ajira wahitimu wote lakini Serikali ipunguze idadi ya wahitimu ambao wanazunguka huku mtaani bila kujua wafanye nini ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Naishauri Serikali kuboresha mfumo wa ajira kama kuna idadi ya wahitimu ambao walishaomba ajira lakini hawakufanikiwa kupata ajira Basi Serikali isitishe kwa muda kuwatangazia wasomi wengine kuomba ajira tena kwenye mfumo wakati wale ambao waliomba nyuma bado hawajaajiriwa.

Kuna sababu gani kuendelea kuwatangazia wahitimu wapya kuingia kwenye mfumo wakati wahitimu wa miaka ya nyuma ambao wameshawahi kuomba ajira mara kadhaa wapo tu nyumbani na hawajui nini hatima yao. Wanaomba ajira mpaka unafika mahali wanachoka wengine wanaamua kuacha kuomba kabisa Yani elimu imegeuka mateso na uchungu.

Naishauri Serikali itoe elimu ya ujasiriamali na somo la menejimenti ya pesa kwa vijana baada ya hapo Serikali itoe mikopo kwa vijana. Mikopo ambayo haina masharti magumu mfano kijana anapohitaji mikopo pasiwepo na masharti kandamizi mfano kupeleka hati ya ardhi au rasilimali nyingine aliyonayo kama mbadala wa yeye kupata mkopo au kuunda kundi la watu watano au zaidi ili waweze kupata hizo pesa.

Ni ngumu sana vijana kutengeneza hilo kundi hii ni kwasababu kila mtu ana ndoto zake na anaishi kwenye hiyo ndoto huwa inakuwa ngumu sana kumpata mtu ambaye anauchungu kama wewe na anandoto ambayo inafanana na wewe. Wakati mwingine kijana hufikiria tufanye biashara ya pamoja itakuwaje mwenzangu akinidhulumu? Hii inasababisha vijana wengi washindwe kufanya ujasiriamali au kujikita katika kilimo na shughuli zingine kwaajili ya kukosa mtaji hatimaye vijana wengi wanaishia kukaa kijiweni asubuhi hadi jioni.

Mabinti wanageuza miili yao kuwa chanzo cha mapato akimpata mwanaume mwenye hela hawezi kukataa ili apate hela ya kununulia mafuta, taulo za kike nk wakati huo mabinti wanasahau kuwa wanaweza kupata madhara ambayo watayatibu kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa na wakati mwingine wanaweza kupata ugonjwa wa UKIMWI, magonjwa ya ngono na hatimaye kupoteza maisha na ndoto zao kuishia hapo.

Vijana wa kiume wanajikita katika kutumia madawa ya kulevya, wizi nk. Naishauri Serikali kuwatazama kwa jicho la pekee wafanyakazi ambao wanajitolea wakiwemo walimu, madaktari, wauguzi nk wafanyakazi hawa wapo ambao wanajitolea na hawapati hata sh 100. Wanaenda kazini kwa nauli, wanarudi kwa kutumia nauli pia. Wananunua vitafunwa wakiwa kazini nk wakati huo mfanyakazi huyo hapati hata sh 100 lakini anafanya Kazi kwa moyo.

Naishauri Wizara ya Afya kutafuta namna ya kuzuia udanganyifu au kuvuja kwa mitihani hasa mitihani ya Leseni kwasababu kuvuja kwa mitihani hiyo kunamuathiri sio mtahiniwa tu bali hata mzazi ambaye anajinyima ili ahakikishe mtoto wake anapata nauli, hela ya malazi, chakula nk ili aweze kwenda kurudia mitihani hiyo. Hali hiyo pia inawaathiri kisaikolojia wanafunzi ambao hawajahusika kwenye uvujishaji wa mitihani hiyo.
 
Vzuri kabisaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom