SoC04 Tanzania tuitakayo iboreshe Elimu, Siasa, Uchumi na masuala ya Kijamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

I_wish2024

New Member
Jun 30, 2024
1
1
Awali ya yote shukrani za kipekee ziende Kwa JamiiForums kwa jukwaa hili lenye lengo chanya katika kufikia Tanzania tuitakayo, katika kuifikia Tanzania tuitakayo nitagusia katika sekta kadhaa ambazo ni Elimu, Siasa, Uchumi na Kijamii.

Mosi, katika elimu kwanza kabisa kuwepo na mapinduzi ya mtaala wa elimu ambao utajikita pia katika vitendo na si nadharia pekee, kupitia hii itawezesha hata vijana wanaohitimu kuweza kuwa na weledi hata wa kujiajiri sawasawa na tasnia wanazosomea katika hatua mbalimbali za elimu.

Pili, viongozi hasa wa kisiasa wawashirikishe wataalamu wao katika sekta husika ili kutokuleta taharuki na wasiwasi Kwa umma kwamfano, labda ni sekta ya Umeme kiongozi mwenye dhamana ashirikishe wataalamu Kwa undani zaidi ili linapokuja suala la kuhusisha umma lisilete taharuki.

Tatu, suala la Uchumi hapa nitagusia upande wa vijana, ambapo miaka ya hivi karibuni kumekuwa na asilimia kubwa ya vijana kutaka kupata mafanikio kupitia njia rahisi na zisizo rasmi matokeo yake ni kuishia kusema ajira ngumu hasa vijana wengi walioko mijini, hata katika Moja ya nukuu za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema "Mtaji wa kwanza ni nguvu zako binafsi" lakini pia katika kuanza Hayati JPM aliwahi kusema anza papo hapo ulipo na si kuhitaji mpaka ufikie kiwango flani maana hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Nne, Jamii inamasuala mengi yanayoikumba hasa katika nyakati za hivi karibuni kwamfano madaya ya kulevya,ushoga, ubakaji, ukatili wa watoto, hofu na matukio ya utekaji na mauaji ya albino ambapo hivi karibuni adha kama hizi zimeanza kujidhihirisha, hivyo basi katika kuifikia Tanzania tuitakayo kwanza kabisa ni lazima elimu zitolewe hasa katika Karne hii ambapo umma au wananchi hawapendi kusoma kwahiyo kutoa elimu kupitia vitabu na machapisho ni sawasawa na kuwaficha hivyo basi inatakiwa kuwepo na mbinu mbalimbali na mbadala Kwa mfano makongamano, semina na mbinu nyinginezo isitoshe katika mitandao ya kijamii pia si wote wanatumia.

Pia katika kuhusiana na malezi ni vyema familia zikawa msitari wa mbele katika kutoa elimu na malezi bora kwasababu familia ndio msingi wa Taifa la Leo na kesho, kama ambavyo inadaiwa kuwa vijana wengi wanaoharibikiwa asilimia kubwa hutoka katika familia zenye mzazi mmoja hasa mama tu (single mother) hivyo wazazi wanajukumu kubwa hasa katika kukemea vitendo hatarishi vinavyotokea majumbani kama vile ubakaji, ushoga na vitendo vinavyoambatana na hivyo.
 
Back
Top Bottom