Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
1)Mabadiliko ni mimi,wewe sisi na wao
Mabadiliko si ndimi,ulimi sema vya kwao
Mabadiliko si ngumi,na kupigana na wao
Vijana youthi asembli,chanzo cha mabadiliko.
2)Vijana ndo nguvu kazi,kijana so lezi lezi
Vijana tufanye kazi,mawazo tuweke wazi
Tusafiri mpaka Swazi,landi tukauze nazi
Vijana youthi asembli,vijana kwazi ni kazi.
3)Tujijue sisi nani,twapaswa kufanya nini
Tunakifanya kwa nini,lini na kwa muda gani
Kwanini tufanye nini,twajiuliza kwa nini
Vijana youthi asembli,tuzalishe mpya fikra.
4)Sana tuwe wabunifu,tuijue sera yetu
Sera isokuwa mfu,ikuze uchumi wetu
Kama ukicheza rafu,utaua nguvu yetu
Vijana youthi asembli,yafundisha ubunifu.
5)Tutumie mitandao,yote ile ya jamii
Tukijenga mtandao,tukizifanya bidii
Biashara mtandao,isambae kwa jamii
Vijana youthi asembli,Ni kioo cha jamii.
6)Tumeshajifunza mengi,tusokuwa tunajua
Sasa tufanye kwa wingi,yale tuliyotambua
Tuvuke hivi vigingi,kesho wengi tutakua
Vijana youthi asembli,imeshaonyesha dira.
7)Karibu wageni wetu,mtembeeTanzania
Muione nchi yetu,jinsi inavyo vutia
Amani ndo vazi letu,katu hatutolivua
Vijana youthi asembli,twatangaza Tanzania
8)Yatupasa kujaribu,kuchoka kwetu ni mwiko
Wala tusione tabu,tuachane na tambiko
Tunayo njema sababu,ya kufanya badiliko
Vijana youthi asembli,ni mimi wewe na sisi
SHAIRI-VIJANA YOUTH ASSEMBLY
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com