Tanzania na Uganda zaingia makubaliano ya kusafirisha shehena kupitia Bandari ya Dar es Salaam

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
755
930
Tanzania na Uganda zimeingia makubaliano ya kuongeza usafarishaji wa Shehena ya Mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Uganda kupitia ushoroba wa Mwanza.

Makubaliano hayo yamesainiwa kati ya Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Prof. Makame Mbarawa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganza Edward Katumba, makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaama

“ Bandari ya Dar es salaam inasafirlisha asilimia Mbili tu ya Mizigo yote inayokwenda Uganda hivyo tumekutana hapa kuingaia makubaliano ya kuongeza usafarishaji wa mizigo” Alisema Mbarawa

Katika kuhakisha mizigo hiyo inasafirishwa kwa kupitia bandari ya Dar es salaam ,serikali ya Tanzania imeendelea kujenga miundombinu muhimu uchukuzi kama vile reli ya mwendo wa kasi SGR, Ujenzi wa Meli katiwa Victoria na ziwa Tanganyaika, aliongezea Mbarawa.

Kwa upande wake Waziri wa ujenzi na Uchukuzi wa Uganda Edward Katumba amesama kuwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam shehena ya kwenda Sudani ya kusini, DRC kongo na Rwanda inaweza kupitia Uganda hivyo ni muhimu kuimalisha usafari wa shehena katika ushoroba wa Mwanza.

Makubaliano hayo yeshuhudiwa na Makatibu wa kuu wa uchukuzi kutoka Uganda na Tanzania pia na wataalama mbalimbali wa wizara hizo.

IMG-20231130-WA1321(1).jpg
IMG-20231130-WA1322(2).jpg
IMG-20231130-WA1320(2).jpg
 
Back
Top Bottom