Tanzania na Hungary kushirikiana katika kuboresha sekta ya maji nchini

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
557
768
1728294308775.jpeg

Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng Mwajuma Waziri wamekutana na Balozi wa Hungary mwenye makazi yake Nairob Kenya Mh.Zsolt Meszaros akiwa na ujumbe kutoka Hungary.

Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za DAWASA Dar Es Salaa kimelenga kupanua wigo wa Mashirikiano na Serikali ya Hungary hususani katika sekta ya Maji.

Aidha, Mheshimiwa Balozi ameeleza ya Kwamba nchi yake inatoa mikopo isiyokuwa na riba kupitia programu ya Hungarian Tied End Credit, l Balozi Zsolt akifafanua zaidi amesema kupitia programu hiyo Tanzania itanufaka eneo la uwekezaji kwenye sekta ya Maji.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemueleza Balozi ya kuwa Wizara ya Maji ipo tayari Kwa ajili ya Mashirikiano katika kuhakikisha lengo la kumtua Mama ndio kichwani linatimia kwani ndio kipaumbele cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.


 
Haya mambo ya ushirikiano tumetoka tunasikia tangu utoto lakini hatuoni unafuu wa maisha
 
Back
Top Bottom