Tanzania mpira unachezwa na waliofeli shule au waliokataa kwenda vyuo; Duniani mpira unachezwa na wale wenye vipaji

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,032
4,731
Mpira unaanza na uwezo wa akili kufanya maamuzi. Mpira unatokana na skills na creativity. Watu wote wenye vipaji wanafaulu katika eneo lao la specialization.

Mafundi simu simu wengi siyo wale waliomaliza degree bali ni wale walio na kipaji chakujifunza kutengeneza simu.

Mafundi furniture siyo wale wenye degree bali wale wenye vipaji waliodharaulika na jamii nakuonekana hawana uwezo wa kukariri na kufauli hesabu, kiswahili, jeografi nk......ila katika fani ya seremala hakuna matumizi ya jeography wala historia.

Tunapokuwa na Taifa ambalo wazazi wanakataza watoto wao kujihusisha na michezo badala yake wakakae darasani kukariri historia ndipo tunapozalisha taifa lisilo na dira.
Tanzania hakuna shule wala chuo cha michezo kinachomilikiwa na serikali.. means tunalazimisha sana kuwa na watu wenye degree ambazo hazina tija kwenye mahitaji ya dunia

Kama tunapenda kuwa na vipaji turuhusu sasa wanafunzi wajikite kwenye vipaji vyao. Tukifanya hivyo tutakuwa na watu wenye talents zaidi ya watu wenye vyeti vya degree zisizozalisha chochote
 
Mzigo wote wa dhambi anaubeba CCM,Hahaha!

Hili halina Mjadala.Full stop
 
Back
Top Bottom