Tanzania Millenials Generation Challenges

audacious

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
240
397
Tujadili kwa pamoja, Je ni changamoto zipi zinazokikabili kazazi cha millenials hususani kwa Tanzania?

Millenials ni kizazi cha watu wote waliozaliwa Kuanzia miaka ya themanini mwanzoni kuja mpaka miaka ya elfu Mbili Mwanzoni. Hichi ndio kizazi kilichobobea na kujikita katika matumizi ya internet, Simu za Mkononi na Matumizi ya mitandao ya kijamii kwa jina lingine huitwa Digital Natives.


Kwa Tanzania pengine na Nchi nyingine za Dunia ya Tatu kizazi hiki kinakumbana na kukabiliwa na changamoto za aina yake .

Idadi ya watu Nchini Tanzania inakadiriwa kufikia watu Millioni 63 mwaka 2022, kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao zaidi ya robo tatu ni vijana Wengi wao wakiwa hawana ajira wala namna yeyote ya kujiingizia kipato.

Kuporomoka kwa uchumu wa Dunia (Great depression )Miaka ya 2007, 2008 pamoja na kuporomoka kwa uchumi kulikotokana na Janga la COVID19 Mwaka 2020 ni pigo lingine linaloathiri maisha ya kizazi hichi.


Kutokana na ugumu huo wa maisha vijana wengi wameshindwa kujenga familia (kuoa na kuolewa) Kama ilivyozoeleka ktk vizazi vilivyopita hivyo kupelekea wimbi kubwa la watoto wanaozaliwa nje ya ndoa wakilelewa na Mama Pekee aka Single mothers.

Kwa miaka ya Zamani haikuwa kawaida kwa kijana anaejituma na kujishungulisha kifikia Umri wa Miaka 40 huku akiwa hajaoa kutokana na ugumu wa maisha na kutokuwa na Muelekeo unaoleweka katika Maisha yake. Kwa siku hizi hili ni jambo la kawaida


Mategemeo ya Wazazi na Jamiii kwa vijana hawa ni Kinyume na Uhalisia wa Maisha wanayoishi hivyo kupelekea Msongo wa mawazo ,kuingia katika mahusiano na ndoa zisizodumu ,kujiingiza katika vitendo haramu ili kuweza kukidhi matarajio ya jamii inayowazunguka nk.

Ukweli ni Kwamba kutokana na Ongezeko kubwa la idadi ya watu ,kutokuwepo na mipango thabit kwa Upande serikali kukabiliana na matatizo ya vijana kwa sasa na mipango Endelevu kwa Siku zijazo ni dhahiri kwamba kizazi hiki na kizazi kijacho cha Tanzania ni vizazi vitakavyoishi katika Tanzania isiyotabirika kuliko kizazi kingine chochote cha Nchi hii kabla na baada ya Uhuru .Kuna kila dalili kwamba jana ni bora kuliko Leo na kesho ni mbaya zaidi ya Leo.

Kizazi cha Taifa letu cha baada ya Uhuru na kabla kidogo ya Uhuru ,kizazi hiki walisoma katika Shule za Serikali huko walilipiwa kila kitu ,walipewa ticket za kusafiri kwenda na kurudi shuleni, walikula mkate wa blue band na chai ya maziwa wakiwa kwenye shule za serikali (Tuliosoma shule hizo mtakubaliana na mimi kwamba siku hizi ktk shule hizo hayo ni ndoto za Mchana) baada ya wao kushika madaraka ya kuliongoza taifa letu Ufisadi na rushwa vilitamalaki, walikwapua mapesa kila waliposhika, watoto wao walisoma ulaya na shule za mchepuo wa kiingereza huko wanalipa mamillioni ya pesa walizoiba katika nafasi walizoaminiwa na wanachi walala hoi.Kazi ya kuendeleza Taifa walioachiwa na waasisi wa Taifa hawakuifanya badale yake waliendeleza Matumbo yao na Familia zao.

Kwakifupi tu niishie hapo na ningependa kufahamu Maoni yako Wewe kijana Mwenzangu, tofauti na nilichoandika Je nini maoni yako ?Ni changamoto zipi zinawakabili vijana kwa sasa na nini kifanyike kukabiliana nazo..

Karibu tujadili..
 
Back
Top Bottom