Acha tuporomoke tu Mkuu kwani hivi sasa nchi yetu ya Tanzania imekuwa ya hovyo hovyo kabisa katika kila Sekta na Idara kuanzia kwa namba moja wetu hadi sisi Visimbilizi tuliopo humu mitaani.
Kwa kweli hii ni hatari sana. Kama taifa tuko kwenye wakati mgumu kweli kweli. Serikali isipokuwa makini nchi inaelekea kubaya kiuchumi; tahadhari ya taasisi kubwa na makini kama IMF siyo ya kubeza ukizingatia Rais wake alikuwa hapa nchini hivi karibuni na "alisifiwa" sana na viongozi ikimaanisha wana imani na uongozi wake.
Kama ndivyo, ni bora wakaichkulia hii tahadhari kutoka taasisi yake kwa uzito mkubwa na wakachukua hatua ASAP.
Kuna uzi nimeuanzisha the same agenda, halafu nyumbu wa lumumba wanabisha
Thread inasema: Mdororo wa uchumi: Rais nashauri Ujiuzulu .
Moderator mkiweza ziunganisheni
Sio uchwara, mbona halisi inaonekana nchini, anzia mfumko wa bei, haijawahi tokea sembe ikawa bei sawa Na mchele, Ni awamu hii tu, sukari nayo bei juu, biashara zinafungwa, makampuni yanafilisika, makampuni yanashindwa kurejesha mikopo Na yanapunguza wafanyakazi, fedha za maendeleo hakuna, mabenk yanayumba, bado tu huoni tunakoelekea siko?
Tatizo utakuwa na akili za kuazima Lumumba