Tanzania kuchangamkia fursa ya ufadhili wa masomo kutoka Umoja wa Ulaya

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,176
760
Tanzania kuchangamkia fursa ya ufadhili wa masomo kutoka Umoja wa Ulaya

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), katika mwendelezo wa ziara yake nchini Hungary, amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. György Hölvényi, Mbunge wa Bunge la Ulaya (EP) kutoka Hungary na Ripota wa Elimu wa Kamati ya Maendeleo ya Bunge la Umoja wa Ulaya.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo ameeleza uhitaji wa kuzitumia vyema fursa za kielimu kutoka Umoja wa Ulaya ambapo Mhe. Hölvényi alieleza kuhusu fursa ya ufadhili wa jumla ya Euro bilioni 8 kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa elimu hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum barani Afrika. Kwa kuzingatia ushirikiano mzuri baina Tanzania na Umoja wa Ulaya, Mhe. Hölvényi alisisitiza ni vyema Tanzania ikachangamkia fursa hiyo ili kuwa miongoni mwa nchi za kipaumbele zitakazonufaika na ufadhili huo.

Aidha, baadhi ya wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wamepanga kufanya ziara nchini Tanzania kuanzia tarehe 23 hadi 26 Februari, 2025 ili kuimarisha ushirikiano baina ya Bunge la Tanzania na Umoja wa Ulaya pamoja na kutembelea miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini hasa miradi ya elimu.
 

Attachments

  • IMG-20250221-WA0123.jpg
    IMG-20250221-WA0123.jpg
    401.9 KB · Views: 1
  • IMG-20250221-WA0125.jpg
    IMG-20250221-WA0125.jpg
    401.3 KB · Views: 1
  • IMG-20250221-WA0129.jpg
    IMG-20250221-WA0129.jpg
    426.7 KB · Views: 1
  • IMG-20250221-WA0133.jpg
    IMG-20250221-WA0133.jpg
    397.4 KB · Views: 1
  • IMG-20250221-WA0135.jpg
    IMG-20250221-WA0135.jpg
    382.1 KB · Views: 1
  • IMG-20250221-WA0137.jpg
    IMG-20250221-WA0137.jpg
    344.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom