Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,588
- 1,190
TANZANIA IWEKEZE UVUVI WA SAMAKI WA VIZIMBA ILI SEKTA YA UVUVI ICHANGIE PATO LA TAIFA KWA ASILIMIA MBILI
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara Mhe. Prof. Sospeter Muhongo mwenye Jimbo lenya jumla ya Kata 21 na Vijiji 68 ambapo Kata 18 ziko pembezoni mwa ziwa Victoria ambao wanajishughulisha na Uvuvi amechangia kwa Umakini wa hali ya juu bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
"Uvuvi unatoa Chakula (Kiuchumi ni food security); Uvuvi unatoa Ajira; Uvuvi unachangia uchumi wa mtu mmoja mmoja; Uvuvi unachangia uchumi wa Taifa" - Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
"Uchumi wa Tanzania kwa miaka 3-4 unakua kwa asilimia 5 mpaka asilimia 6 (asilimia 5.6), kwenye hili Bunge la Bajeti tutoe ushauri kwa Serikali kusudi Uchumi wetu uweze kuondoa umasikini kwa sababu uchumi lazima ukue kuanzia asilimia 8 kwenda asilimia 10" - Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
"Sekta 5 tu ndizo zinaweza kufanya uchumi uende kwa haraka (Accelerated Growth); Gesi Asilia, Madini, Kilimo, Mifugo na Uvuvi & Utalii. Hizi Sekta 5 kila moja ingechangia asilimia 2 ya ukuwaji wa uchumi tungeweza kufika asilimia 8 mpaka asilimia 10" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Watalaam wa lishe wanasema kwamba kama unataka Mlo Kamili (Balanced Diets) chakula bora unapaswa kutumia grams 280 kwa wiki. Siku ya kwanza grams 140 na siku nyingine grams 140" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Duniani kuna watu takribani Bilioni 8, Tanzania ikiuza huko Samaki tutapata fedha nyingi. Kama soko la Tanzania ni ndani ya Bara la Afrika lenye watu Bilioni 1.43 tunaweza kupata fedha nyingi sana kwa hizo grams 280. Sekta ya Uvuvi tuichukulie kibiashara" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Mwaka 2022 Samaki waliozalishwa Duniani walikuwa ni Tani Milioni 184.6. Mzalishaji wa kwanza alikuwa ni China 🇨🇳 (Tani Milioni 67.5, tani Milioni 54.6 alizalisha kwa kutumia Vizimba); Pili alikuwa ni India 🇮🇳 ambaye uzalishaji wake Duniani ni Tani Milioni 7.56. Maoteo ya mwaka huu ya biashara ya Samaki Duniani mapato yake yatafika Bilioni 612 na hapo ndipo tunapaswa kuishawishi na kuishauri Serikali iwekeze zaidi kwenye Uvuvi" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Samaki wa Vizimba Duniani wanaozalishwa ni tani Milioni 180. Mzalishaji namba moja ni China 🇨🇳 ambaye anazalisha theluthi moja (1/3), wa pili ni India 🇮🇳 ambaye anachuana na Misri. Kwa Afrika Misri ndiyo anaongoza" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Mwaka 2021 Misri ilizalisha Samaki tani Milioni 2.2, kati ya hizo tani Milioni 1.7 walizalisha kupitia Vizimba ambayo hii ni zaidi ya asilimia 77. Wengi wamesema Samaki wamekosekana Ziwa Tanganyik, Nyasa na Victoria. Suluhisho lake ni uvuvi wa Samaki wa Vizimba" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Ziwa Tanganyika umri wake ni miaka Milioni 10, Maji yaliyomo Ziwa Tanganyika ujazo wake ni Mita za ujazo 18,880 na aina ya Samaki waliopo ndani ya Ziwa Tanganyika ni zaidi ya 350" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Ziwa Nyasa lina umri wa miaka Milioni 2, ujazo wa Maji kwenye Ziwa Nyasa ni Kilomita za ujazo 8400. Ziwa Nyasa lina aina nyingi za Samaki kuliko Maziwa yote Duniani ambapo lina kati ya Samaki 800 mpaka 1000 (aina za Samaki - Species of Fishes)" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Ziwa Victoria lina umri wa Miaka Laki Nne, Ujazo wake wa Maji ni Kilomita za Ujazo 2224, Aina ya Samaki waliomo Ziwa Victoria ni zaidi ya 500" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Kenya 🇰🇪 wana asilimia 6 ya Ziwa Victoria, Uganda 🇺🇬 wana asilimia 45 na Tanzania 🇹🇿 tuna asilimia 49. Kenya ina Viwanda 18 vya Samaki, Uganda wana Viwanda 11. Tanzania Musoma hakuna kiwanda hata kimoja cha Samaki" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo
"Tuwekeze kwenye Uvuvi wa Vizimba, tutoe mikopo. Tutoe mikopo kwa watanzania waanzishe Viwanda vya Samaki kwa sababu Samaki wa Vizimba watakuwa wengi" - Mhe. Prof Sospeter Muhongo