Niliwahi kuuliza na nauliza tena.
1. Je kiongozi wa majuha anakuwa ana akili kidogo au ni juha zaidi?
2. Kiongozi wa werevu anakuwa mwereve kiasi au mwerevu zaidi?
Ukitizamana kwa umakini sana Tanzania ina wananchi majuha wengi pengine kuliko Kenya na Uganda. Wananchi wengi wa Tanzania hawajui siasa na hawafuatilii kabisa siasa ila wanafuatilia wanasiasa wanapokuwa majukwaani tofauti na nchi za wenzetu wenye akili ndo huenda kwenye mikutano ya siasa lakini kwa nchi yetu wapuuzi au wajinga ndo huwa wanaenda kwenye mikutano na hivyo hawa hushangilia kila ambalo wanasiasa husema haijalishi kama lina manufaa au halina manufaa.
Na hili limekuwa tatizo kubwa ambalo limesababisha viongoz wabovu wawe wanafanya maamuzi mabovu na bado wakshangiliwa kana kwamba wamefanya jambo la msingi.