Tanzania imeanzisha Majaribio ya Ujenzi wa Barabara kwa Teknolojia ya Armarseal

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
573
781
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha miradi ya majaribio (pilot projects) kwa ajili ya matumizi ya teknolojia mpya katika ujenzi wa barabara ikiwemo Armarseal.

Teknolojia hii inalenga kuboresha uimara wa barabara na kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara.

Moja ya Mradi huu wa majaribio umefanyika kwenye barabara ya Mtwara-Mnivata-Newala-Masasi, ambapo kilometa 12 zimefunikwa kwa lami maalum inayosaidia kuziba nyufa na kuimarisha kokoto za barabara, hivyo kuongeza muda wa matumizi ya barabara kwa miaka mingi bila kuhitaji matengenezo makubwa.
IMG_20250213_095736_474.jpg

Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Doto Chacha John na kusisitiza kuwa, mradi huo wa majaribio unalenga kutatua changamoto kubwa ya uharibifu wa barabara kutokana na maji, ambayo yamekuwa adui mkubwa wa miundombinu ya barabara.
IMG-20250213-WA0001.jpg

“Kwa kutumia Armarseal, barabara zitalindwa kwa kuzibwa nyufa na kuimarisha kokoto zilizopo ili zisilegee, hatua inayotarajiwa kuongeza muda wa matumizi ya barabara hadi miaka 15 hadi 20 bila uharibifu mkubwa,” alisema Mhandisi Chacha.
IMG-20250213-WA0002.jpg

Mradi huu unatekelezwa na mkandarasi mzawa RAHIMY CO. LTD, kwa kushirikiana na kampuni ya Jobling Purser kutoka Uingereza. Gharama ya mradi inakadiriwa kufikia shilingi milioni 863.1.

Kwa upande wake Faisal Malik Mahsen kutoka RAHIMY CO. LTD, amesema Tanzania ni kati ya nchi chache zinazofanya majaribio kutumia teknolojia hii, ikiwa ni ya tano kwa Afrika.
IMG-20250213-WA0003.jpg

"Kwa kupitia upembuzi yakinifu, tumejiridhisha kuwa hii ni suluhisho la muda mrefu kwa changamoto ya uharibifu wa barabara. Hakuna kokoto itakayotoka wala maji kuingia ndani ya kokoto," alisema na kuongeza

"Ningeshauri barabara zote Tanzania zitumie teknolojia hii ya Armarseal ili kuzilinda na kupunguza gharama kubwa za matengenezo."
IMG-20250213-WA0004.jpg

Katika kufanikisha mradi huo, mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta na uongozi wa Mkoa wa Mtwara umetajwa kuwa ni wa muhimu kwa kutoa ushirikiano wa karibu kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi, huku wananchi wa eneo hilo wakielezea matumaini yao kwa maboresho ya miundombinu.
IMG-20250213-WA0005.jpg
IMG-20250213-WA0006.jpg
 
Mimi na technology ya kujenga barabara itakayodumu miaka 100 ni ya mfumo wa interlock pannelblock ni block zinazotengenezwa kwa mchanganyiko wa taka za plastic na mchanga haipitishi maji Wala fungas na unajenga popote hata sehemu zenye unyevu.

Barabara isiyotumia lami bali ni taka za plastic na mchanga zinayeyushwa kisha ugandishwa pamoja kwenye model ili kupata wallblock ambazo ni interlocking so unapanga barabara huku ikiendelea kutumika unapanga kama pavers zenye upana wa mita nne urefu inategemea na upana wa barabara.

Gharama ya barabara ni million 400 kwa kilometer moja badala ya sasa ya lami kwa bilioni moja kwa kilometer then hata miaka kumi haifiki.

Hii yangu ina uwezo wa kubeba tani 150 so hakuna haja ya kuwepo vituo vya mizani ili kulinda barabara.
 
Back
Top Bottom