Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,684
- 20,581
Ndugu zangu Watanzania,
Kumekuwa na utamaduni na tabia ya baadhi ya watanzania wachache wenye wivu na chuki binafsi za kuchukua picha mitandaoni kutoka Nchi za nje ya Tanzania na kuziweka mtandaoni na kusema ni Tanzania.
Picha hizo zimekuwa ni zile zenye kuchafua Taswira nzuri ya maendeleo na mafanikio tuliyoyapata na kufikia kama Taifa. Imekuwa ni kawaida kuona mtu anachukua picha ya wanafunzi au kipande cha barabara kibovu na kisicho pitika kutoka nchi fulani barani Afrika Na kusema ni Tanzania.
Lengo likiwa ni kuichafua na kuipaka Matope serikali yetu na kuonyesha kuwa haifanyi kazi. Jambo ambalo siyo la kweli hata kidogo. Kwa kuwa Watanzania wote wanafahamu namna serikali ilivyofanya kazi kubwa ya kusogeza huduma za kijamii karibu kabisa ya Mwananchi zenye ubora wa kiwango cha juu.
Kuna picha hiyo hapo juu watu wameiweka mtandaoni ikionyesha wanafunzi waliovalia sare nyekundu kwa upande wa sketi na suruali pamoja na shati jeupe na kusema kuwa ni Tanzania wakiwa wamekaa kwenye matofali na darasa bovu la miti na lililokandikwa kwa udongo huku likiwa linapitisha Maji Matupu chini . Jambo hilo ni la uongo kwa sababu hakuna sare ya aina hiyo inayotumika na kuvaliwa na wanafunzi katika shule za serikali kwa upande wa shule za Msingi.
Rai yangu ni kuwaasa na kuwataka watanzania kuacha tabia hiyo mbaya na isiyokubalika ya kuichafua na kuipaka Matope serikali yetu kwa chuki binafsi. Tuache kueneza upotoshaji na habari za uongo kwa malengo Binafsi. Tuendelee kuiunga Mkono serikali yetu na kushiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na kulinda Miundombinu na miradi ambayo imekuwa ikijengwa kila kona ya Nchi yetu pasipo kumchangisha hata mia Mwananchi.
Embu Tazama hapa kama Sample Namna serikali yetu ilivyojenga shule kwa ubora na kuvutia Utafikiri ulaya pasipo kuomba michango kutoka kwa watanzania.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.