Hakika watanzania wa wakati ule wa uhai wa Kipenzi chetu Waziri mkuu wetu Hayati Edward Moringe Sokoine tuliamini kuwa Mh.Sokoine angeupata Urais wa nchi hii, angejenga misingi ya utawala bora na mambo kama rushwa ufisadi visingekuwepo.
Leo lakini masikini watanzania Mungu alimpenda zaidi Mh.Sokoine na ndoto zake hazikutimia na nchi ikaingia kwenye Wizi, Rushwa na Ufisadi ambao mpaka umetufanya watanzania tuwe masikini wa kutupwa. Wachache ndio matajiri wakiongozwa na viongozi wetu ambao tuliamini wangemuezi Mh.Sokoine ambaye hakutamani Utajiri amekufa akiacha Shati 3, Na pea 2 za viatu hakuacha Nyumba Kule Oysterbay wala Mikocheni Wala Masaki au Upanga.
Watanzania tuache kumwezi Hayati Sokoine Kwa mzaha eti alikataa maovu wizi rushwa Na ufisadi.Viongozi wetu kwenye mioyo yao hawako hivyo .Viongozi wetu wamefikia hatua ya kuiba na kuficha fedha ambazo in Kofi za masikini nje ya nchi, viongozi wetu wa majumba mpaka nje ya nchi inauma sana.Kama kweli tunasema tunamuezi Hayati Sokoine Kwa vitendo basi tuwe tayari kuishi kama alivyokuwa anaishi , anazunguka nchi nzima usiku Na mchana kujua shida za wananchi .
Rasilimali za nchi alitaka ziwe zetu wote.Binafsi siamini kama viongozi wetu wanamkaribia Hayati Sokoine Kimatendo.EWE MWENYEZI MUNGU IPE PUMZIKO LA MILELE ROHO YA ALIYEIPENDA NCHI YAKE NA WATU WAKE HAYATU SOKOINE AMEN.