Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 220
- 181
TANZANIA HAINA MUFTI !
TANZANIA HANA SHEKH MKUU!
Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kiongozi mkuu wa taasisi ya kidini iitwayo Baraza kuu la waislamu wa Tanzania bara akitajwa kama mufti na sheikh mkuu wa Tanzania na mtazamo huu ni makosa makubwa sana na uamebeba maudhui ya upotoshaji kwa kumvika mtu cheo ambacho kiuhalisia hakipo na hakiwezekani kuwepo kwa sababu zifuatazo;
..... Inaendelea.
3️⃣ Sababu ya tatu kwanini Tanzania haina Mufti wala sheikh mkuu ni kwakuwa vilevile serikali ya Tanzania haina dini maalumu inayofuatwa na serikali na imeruhusu watanzania wafuate dini wanazozitaka.
Swala la kuabudu na kuwa na dini lipo nje ya shughuli na majukumu ya kiserikali.
Watanzania wamegawanyika katika dini na madhehebu yenye taasisi tafautitafauti.
Waislamu wapo madhehebu tafauti tafauti na chini ya kila dhehebu kuna taasisi tafauti tafauti zilizosajiliwa serikalini.
Baadhi ya madhehebu ya dini ya kikristo/kikristu hapa Tanzania ni Roman Catholic, Lutheran, Anglican, Pentecostal, wasabato nk. Sasa wakristo wao wanapotajwa viongozi wao utasikia ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI MKOA WA DAR ES SALAAM, DAYOSISI FULANI, PAROKIA AU USHARIKA FULANI!
Walutheri hivyohivyo utasikia ASKOFU WA KKKT ( Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania ) Kanda au dayosisi ya mashariki nk.
Upande wa wasabato hivyo atatajwa kuwa ni mchungaji wa kanisa la kisababto, au la kipentekoste, la ufufuo na uzima nk.
Hatujasikia kuwepo ASKOFU MKUU WA TANZANIA bila kutaja wa kanisa gani, na eneo gani!
Wala hatujasikia KARDINALI MKUU WA TANZANIA bila kuongeza kwamba ni wa kanisa katoliki.Hata papa wa huko vitikani hutajwa kama KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI , SIO KIONGOZI WA DUNIA AU KIONGOZI WA WAKRISTO WOTE DUNIANI.
Kiongozi wa KANISA KATOLIKI.
Kila kinasa linapomtaja kiongozi wake lazima wataje na jina la kanisa analoliongoza na Kanda,mkoa, parokia, dayosisi au kigango anachoongoza.
Ni BAKWATA PEKE YAKE INAYOMTAJA KIONGOZI WAKE MKUU KAMA MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA kama vile watanzania wa dini zote na madhehebu yote wako chini yake!
Ni bakwata peke yake inaowataja viongozi wake wa mikoa kama MASHEIKH WA MIKOA bila kutaja wa dini gani au madhehebu na taasisi gani kama vile raia wa dini zote waliomo kwenye mkoa huo wapo nyuma yake!!.
NITOE MFANO.
Ukisema jaji mkuu wa Tanzania tunaelewa kuwa unamzungumzia kiongozi anayewatumikia watanzania wote wa dini , madhehebu, makabila na vyama vyote vya kisiasa na kijamii katika sekta ya mahakama chini ya wizara ya katiba na sheria Tanzania nzima.
Ukisema mkuu wa mkoa wa Mwanza unamaanisha mtu anayemuwakilisha mh Rais katika mkoa wa Mwanza akiwa mtumishi wa watu wa dini, madhehebu, makabila na vyama vyote!.
Ukisema mwenyekiti wa CCM taifa, mkoa au wilaya tunajua unamzungumzia kiongozi wa chama maalumu cha siasa anayewaongoza wanachama wa chama hicho katika nafasi iliyotajwa na sio kiongozi wa watanzania wote.
Upande wa taasisi za kidini ni hivyo hivyo lazima itajwe taasisi hiyo na nafasi ya kila muhusika.
Nimetoa mifano ya taasisi za kikristo hapa Tanzania zinavyowatambulisha viongozi wake.
Ni BAKWATA PEKE YAKE ambayo viongozi wake utasikia MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA.
JE ni mtumishi wa watanzania wote kama ilivyo JAJI MKUU WA TANZANIA?!
Je Mufti wa Tanzania anafanya kazi chini ya wizara gani na kwa sheria gani?!
Ili kuweka mambo sawa kuna nukta zifuatazo .
A. Kwakuwa taasisi hii haina wala haitakiwi kuwa na ofisi Zanzibar kwa kuwa Tayari waislamu wa zanzibar wanayo taasisi inayosimamia mambo yao ya kidini chini ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar jina la taasisi hii yatakiwa liwe BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANGANYIKA
( au Tanzania bara)
B. Yatakiwa kiongozi wao mkuu ajulikane kama MUFTI NA SHEIKH MKUU WA BAKWATA na siyo mufti na sheikh mkuu wa Tanzania.