Je wewe ni digital artist wa kitanzania au ungependa kuingia katika profession hii? Nimeanzisha online community ambayo nategemea itakuwa msingi mzuri utakaosaidia kujenga mazingira ambayo watu watashare mawazo, ujuzi, rasilimali na pia sehemu ambayo itatoa nafasi za watu kupata kazi mbalimbali zinazohusiana na industry hii zitakapojitokeza.
Hii community inawahusu:
Graphic Designers
Photographers
Animators (+modelers, riggers, painters, texture artists)
Video Editors
Video Producers/Directors
Screenwriters
Music Producers (+ Audio Engineers)
Visual Effects Artists
Game Developers
Computer Programmers
Media Houses
Category zingine zitaongezwa kulingana na maoni ya wadau
Nina mawazo mengi ya jinsi hii community inaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa members na ni matumaini yangu wazo hili limeeleweka na litapokelewa vizuri. Kama una maswali, ushauri au maoni, uko huru kuyatoa.
Kwa sasa nimefungua facebook page lakini wadau watakapoanza kujitokeza tutaanza discussion rasmi ya mambo mengine yatakayofuata.
www.facebook.com/digitaltanzania
Paschal Paul (P.P.R)
Ps. Nimefanya kazi katika industry hii kwa karibu miaka 8 na ninamiliki kampuni ya mambo ya production.