Tanzania bado giza nene

GIBRALY

Member
Mar 14, 2017
31
35
TANZANIA BADO GIZA NENE.

Nakumbuka tulinunua ndege mbili aina ya BOMBARDIER gharama za ndege mbili (2) ni 1.6 trilioni sasa ndege hizi zinamekusanya billioni 9 kwa kipindi cha miezi 4 katika report ya hivi karibuni ina maana ndege mbili kwa mwaka zitakusaya bilioni 27 kwa miaka kumi zitakusanya bilioni 270 Kwa miaka 30. Ndege (2) zitakusanya bilioni 810 Kwa miaka 60 ndege mbili zitakusanya trioni 1.620 yaani bilioni 1620 SASA ONDOA GARAMA ZA MATENGENEZO NA MATUMIZI MENGINE.

Gharama ya ndege zetu tulizonunulia zitarudi baada ya miaka 60. Mhhh hii ni biashara ambayo tumewekeza na inatakiwa shirika lijiendeshe kama Rais Magufuli alivyosema. Nimetoa mfano yaani ili hilo shirika liweze kununua ndege nyingine moja itachukua miaka 30. Tuweni wavumilivu ktk uchumi huu wa viwanda lakini kumbukeni 80% ya barabara zetu hazipitiki wakati wa mvua.

Haya ni maoni tu.
 
Kama hujui in vyema ukauliza.Muulize upya aliyekueleza bei ya bombardier.Lakini pia uliza wafanyabiashara wenye ufahamu wakueleze namna biashara inavyokwenda.Biashara inavyoanza inakuwaje na ikikomaa inakuwaje.ATCL ndiyo inaanza unataka iingize sh.ngapi?.Kwa maelezo yako hayo unamaanisha biashara ya Ndege haina faida.Kawaulize Ethiopia wakueleze.Ethiopia Airlines ndiyo inaendesha uchumi wa nchi.Halafu,Ndege zinaleta fedha nyingi tu.Kaulize Airport na TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…