Tangu Soka lianze hadi leo hii, Kuna Mchezaji yeyote aliyefikia kiwango cha Maradona au Messi?

Buenos Aires

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,894
1,622
WADAU WENZANGU HESHIMA KWENU!

1-LEONEL ANDRES MESSI-LA PULGA


2-DIEGO ARMANDO MARADONA-GOLDEN BOY



Tangu soka lianze hapa ulimwenguni. Ni mchezaji yupi aliyefikia kiwango cha wafalme hawa wa soka hapa duniani Al maarufu LEONEL ANDRES MESSI-LA PULGA & DIEGO ARMANDO MARADONA-GOLDEN BOY

Nataka tu niwakumbushe wadau wenzangu! Najuwa kuna wengine watakuja hapa na misemo tofauti tofauti na mada isemavyo flani anamagoli mengi la hasha! hapa hatuzungumzii wingi wa magoli bali tunazungumzia viwango bora vya mchezaji!

MESSI na Maradona wanajulikana ni wachezaji wa kipekee mno kuwahi kutokea katika ulimwengu huu wa soka, wamepitia wakati mgumu sana,

Tofauti na kipindi cha akina PELE Wamecheza katika kipindi ambacho watu hawakuwa wakijua sana mpira tofauti na sasa, na hata sheria zilikuwa laini Mno tofauti na sasa Sheria zimekuwa ngumu kitu kidogo filimbi, hebu fikiria kuwa kipindi hicho OFF-SIDE zilikuwepo za kumwaga , hata ukimpa mtu ki-pepsi ilikuwa ni poa tu, ukimpiga mtu push ya nguvu jambo la kawaida REFA hakufikirii kama sasa.....

Vile vile ufungaji ulikuwa ni mrahisi mno, magoli yalikuwa sio magumu kama ambavyo tumewashuhudia katika kipindi chao.


Pia ningeomba tuwe wakweli bila kuwa na ubaguzi wa aina yeyote ule.. eti kwa sababu huyu White tusimpe haki yake, eti kwa sababu huyu ni Black tusimpe haki yake..... No! hiyo haipo... na kama mtu huyo atachagua mchezaji kwa kigezo cha rangi ama utaifa wake basi huyo atakuwa si mshabiki haswaa wa soka. Kila mchezaji tumpe haki yake awe mweusi ama mweupe na vilevile taifa alikotoka.

Ahsanteni;
 
Sasa kama kipindi Cha Pele ukimpiga mtu kipepsi ilikua kawaida, faulo ilihesabiwa toka kiunoni kwenda juu, ukipigwa push ya kudhamiria Hamna faulo, huoni kuwa Pele alikua bora kwenye mazingira magumu? Wachezaji WA sasa kina Messi wamekuta mpira umekua rahisi Sana!
 
Umri wangu n Mara mbili ya ulionao.
Okay mi umri wangu 52...hivyo wewe una 104

-Tuendelee....why uwakatae wawili hawa wafalme wa soka? Una evidence yeyote?

-Na yupi unayemkubali zaidi yao? Maana hukuja na jibu linaloeleweka, naweza nikasema wewe ni mwanafunzi mambo haya waachie wenyewe wanaolijua soka sawa bwana mdogo? Naomba ujibu swali hapo juu
 
Nimejibu swali. The question wasn't statistically asked. Kama ni kwa ufungaji magoli Pele anawazidi zaidi hawa wawili,kama ni ball control ndo kwanza hata nusu ya Ronaldinho hawajafikia. Kwa maisha magumu,C.Ronaldo kateseka Sana. Maisha magumu mno.

Kama unasemea kuwa magoli yalikuwa ni marahisi kufungika basi tusiwewajudge kama ndo the best maana bado soka litaendelea kuwa gumu na ufungaji utakuwa mgumu....
NB: Usiniulize tena maswali mm siyo mwanafunzi wako badala yake omba ufafanuzi.
 

Hujaielewa mada bali umekurupuka tu, mleta uzi kauliza.. Tangia soka lianze hapa ulimwenguni je! Ni mchezaji yupi aliyefikia kiwango cha wafalme hawa wa soka hapa duniani Diego na Leo? Sasa wewe umekuja na majibu tofauti kabisa! Mara cjui pele ana magoli mengi, mara cjui ball control gaucho,mara sijui Cr7 kateseka sana, maisha magumu mno! Hahahaaa hueleweki.... Rejea kuisoma upya mada kisha uje na majibu yanayo eleweka!


Mi nitakusaidia kidogo chagua mchezaji unaye mkubali aliyewazidi messi na Diego, i mean uje na jibu moja tu,
 

Kalale kama akili yako inakutuma kwamba mchezaji atakuwa bora bila vigezo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…