Tovuti hiyo ina ujumbe wa Kiingereza ulioandikwa vibaya unaotafsirika: "Kasome Nchini Norway Kozi Yoyote Uliyochagua Bila Malipo kwa Muda wote wa programu"
"Programu ya Scholarship ya Chuo Kikuu cha Bergen Huwawezesha Wanafunzi wa Kimataifa Kusoma nchini Norway kwa Raha na Bure. Waombaji wajaze fomu hapa chini na kubofya Omba,”
Tovuti hiyo ambayo ina muonekano wa kutilia shaka (norway.visa2abroad.online) imechapisha “nafasi” hizo kwenye makundi ya mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, na katika nchi kadhaa ikiwemo Tanzania.
Tovuti hiyo pia inaonesha "fomu ya maombi" ambayo inataka muombaji kujaza taarifa binafsi kama vile jina, barua pepe, nchi anayoishi na kozi/programu ambayo anakusudia kusoma.
- Tunachokijua
- Kwenye matangazo yao yanayoonekana mtandaoni wanaonesha ufadhili wa Chuo Kikuu cha Oslo nchini Norway, huku maelezo yakieleza chuo kinachohusika na scholaships hizo kuwa ni Chuo Kikuu cha Bergen.
Suala hilo linaleta mkanganyiko na kuondoa kabisa imani na tangazo hilo kwani vyuo hivyo vinabeba majina ya miji miwili tofauti nchini humo. Oslo ni mji mkuu wa Norway, na Bergen ni jiji la pili kwa ukubwa na kuna umbali wa takribani kilomita 460 kati ya miji hiyo miwili.
Pia inatia mashaka kwamba ufadhili wa masomo halali ungetangazwa kwenye tovuti iliyoundwa vibaya na maandishi yaliyoandikwa vibaya. Hivyo, inatia shaka kuwa tangazo hilo limetolewa na taasisi ya elimu ya juu.
Suala lingine ni kuwa ukibofya maneno “APPLY NOW” hata bila kujaza taarifa zozote tovuti hiyo inaleta ujumbe wa kupongeza kuwa maombi yametumwa. Hili ni jambo lingine la kutilia shaka.
Hata hivyo, tovuti hiyo haitoi kiunganishi chochote cha tovuti za Chuo Kikuu cha Oslo na Chuo Kikuu cha Bergen. Hii ni dalili kwamba hakuna uhusiano wa kweli na vyuo vikuu hivi au udhamini wowote unaotolewa nao.